DED wa Busega Khamis Yunah akisisitiza jambo kwa watumishi ambao awaonekani pichani. |
Na Shushu Joel,Busega.
MKURUGENZI wa halamashaul ya wilaya ya Busega(DED) Khamis Yunah.amesema kuwa wakati Rais wa Jamhuli wa muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipambana na rushwa kubwa na matumizi mabaya ya madaraka kwavigogo,ofisi yake nayo imeanza kupambana na mambo hayo kwa wafanya kazi wake.
Alisema kuwa wakati Rais Magufuli akitumbua majipu makubwa yeye kwa upande wake atatumbua majipu madogomadogo ili kuweka nidhamu ya kazi kwa wafanyakazi iweze kuwepo na pia hata kuizidi ilie kauli mbiu ya Rais ya hapa kazi tu.
Yunah aliyasema hayo alipokuwa na kikao kazi ambacho pia kiliwashilikisha watendaji wa kata na vijiji,wafanyakazi wa afya,wakuu wa idara,maafisa kilimo kata na wenyeviti wa vijiji kilichofanyika katika kijiji cha Bulima,kata ya Nyashimo wilayani Busega, chini ya mkuu wa wilaya hiyo,Paul Mzindakaya.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa mtumishi yeyote Yule wa serikali katika halmashaul hiyo ambaye hatoweza kwendana na kasi anayoinyesha Rais Magufuli hatutomvumilia hata kidogo na wala hata kumuonea haya yeyote ile katika utendaji wa kazi za halmshaul hizo.
Aidha Yunah alisema kuwa hayuko tayari kumfumbia macho mfanyakazi wake ambaye ataonyesha zaili kashindwa kuondena na kasi ya Rais ni bora akajiondoa kabisa mapema katika kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi kwa wakati Hivyo siko tayari kuwajibishwa kwa kuwafumbia macho watumishi au wasaidizi wengine katika halmashaul yangu alisema Yunah.
Aliwata watumishi hao kuwa na nidhamu ya hali ya juu kazini,kuhudumia wananchi vile ipasavyo na kwa muda mwafaka, kuwa waadilifu ikiwa na na kuheshimu matumizi pia matumizi ya fedha za umma.
Aliongeza kuwa kila mtumishi anatakiwa kuwa tayari na mabadiliko ambayo tayari yamesha anza kuonekana na pia kuondoa fikra ambazo watakuwa nazo.
N kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Paul Mzindakaya aliwata watumishi wote ndani ya wilaya yake kuiweza kutambua wajibu wao walionao katika kutimiza majukunu yao katika kuwatumikia wananchi .
Mzindakaya aliongeza kuwa naye kwa upande wake yuko tayari kutumbua kila aina ya jipu lolote lile liwe gumu au jepesi nah ii ni kutokana na kasi iliyopo sasa katika nchi yetu chini ya Rais Dkt Magufuli, Hivyo amempongeza Dkt Magufuli kwa kasi aliyoionyesha na kumtaka aweze kuongeza nguvu zaidi ili kupambana zaidi na kwa upande wangu nitaanza kwa kutoa mifano kwa yeyote atakayekeuka kasi iliyopo sasa alisema.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.