ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 10, 2015

VITENDO VYA UDHALILISHAJI NA UBAKAJI WATOTOTO WILAYA YA TEMEKE VYAONGEZEKA

 Mkuu wa Dawati la Jinsia katika Kituo cha Polisi Mkoa wa Kipolisi Chang'ombe, Thecla Kitajo.
 Mkuu wa Dawati la Jinsia katika Kituo cha Polisi Mkoa wa Kipolisi Chang'ombe, Thecla Kitajo (kulia), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo mchana, ambao wanatembelea vituo vya polisi na masoko ya Manispaa za Ilala na Temeke kujionea jinsi vitendo hivyo vilivyo pungua baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG) kutoa mafunzo ya kupinga ukatili huo katika maeneo hayo. Kushoto ni Ofisa wa Polisi wa Dawati la Jinsia wa Kituo hicho, Meshack Mpwage.
 Ofisa wa Polisi wa Dawati la Jinsia wa Kituo hicho, Meshack Mpwage, akizungumza katika mkutano huo.
 Ofisa wa Jeshi la Polisi wa Kituo cha Chang'ombe, Digna Ngatena (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mwanasheria wa Shirika la EfG, Grace Mate)
Maofisa wa Jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia wa Kituo cha Polisi Chang'ombe. Kutoka kushoto ni Albentina Aloyce, Nuni Munisy na Rose Lukanga.

Dotto Mwaibale

WAKATI vitendo vya ubakaji na udhalilishaji kwa watu wakubwa vikipungua matukio ya vitendo hivyo kwa watoto wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam vimekuwa vikiongezeka kila siku.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Dawati la Jinsia wa Kituo cha Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke Chang'ombe Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Thecla Kitajo wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, ambao wanafanya ziara katika masoko ya Manispaa ya Ilala na Temeke na vituo vya polisi kujua vitendo vya ukatili wa kijinsia ulivyopungua katika maeneo hayo baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG), kutoa mafunzo ya kupinga ukati huo.

"Vitendo vya ukatili wa kijinsia na ubakaji kwa watu wakubwa umepungua kwa kiasi fulani lakini kwa upande wa watoto bado tunachangamoto kubwa kwani kila siku tunapokea kesi ambapo kwa mwezi tunapokea matukio zaizi ya 25 na zaidi" alisema Kitajo.

Kitajo alisema hali hiyo inatokana na watoto hao kufanyiwa vitendo hivyo na watu wazima ambao wengi wao ni jamaa zao wa karibu na tabia ya wazazi kuwa mbali na watoto wao.

Alisema licha ya Jeshi la Polisi kujitahidi kufuatilia kesi hizo lakini zimekuwa zikiishia njiani baada ya wanaotakiwa kutoa ushahidi kushindwa kufika mahakamani kwa hofu ya watenda kosa ambao ni wapenzi na hao walifanyiwa vitendo kuja kungwa na sababu za kifamilia.

Alisema vitendo vya udhalilishaji na ubakaji vitakwisha iwapo tu jamii itavikataa kwa nguvu moja badala ya kuliachia jeshi la polisi kuvishughulikia.

Ofisa wa jeshi hilo  wa dawati hilo, Meshack Mpwage alisema umaskini na mambo mengine kama ya mgeni akifika nyumbani na kulazwa na watoto pia unachangia kwa kiasi kikubwa watoto kubakwa.

"Wazazi wamepanga vyumba viwili cha kwao na watoto mgeni akija anapangiwa kulala na watoto hukuo chumbani mgeni huyo anaamua kuwadhalilisha watoto au mtoto" alisema Mpwage

Mpwage alisema tabia ya ubize kwa wazazi pia ni moja ya sababu inayowawafanya watoto wakikutwa wamekwisha haribika kwa vitendo hivyo kwa sababu ya wazazi wao kuwa mbali nao na kushindwa kujua kinachoendelea dhidi yao.

Alisema hivi sasa changamoto kubwa ya watoto ipo kewa madereva taksi ambao wazazi wanawatumia kuwapeleka mashuleni na madereva bodaboda ambao uwashawishi watoto hao kwa kuwapa chipsi na fedha chini ya shilingi 1000 na kuanza kufanyanao mapenzi.

Mpwage alitoa mwito kwa kila mtu kujengea tabia ya kupiga vita vitendo hivyo vya udhalilishaji kwa kutoa taarifa polisi jambo litakalo saidia kupunguza vitendo hivyo kama sio kuvimaliza kabisa.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.