Michezo ya robo fainali ya michuano ya kombe la Cecafa Chalenji Cup imetimua vumbi hii leo huko Adis Ababa Ethiopia ikishuhudia timu ya Tanzania bara The Kilimanjaro stars ikiyaaga mashindano hayo.
Katika mchezo wa kwanza timu ya taifa ya Uganda the cranes imesonga mbele mara baada ya kuwagagadua wanyasa wa Malawi bao 2-0, huku timu ya Tanzania bara maarufu kama The Kilimanjaro stars ikiondoshwa na Wenyeji Ethiopia kwa penati 4-3 hii ikija mara baada ya kushuhudia dakika 120 za sare ya 1-1.
Robo fainali ya pili itapigwa hapo jumanne Desemba mosi kwa Sudan kusini kukipiga na Sudan,Rwanda wakipepetana na Kenya.
Michezo ya nusu fainali itafanyika siku ya Alhamisi huku mchezo wa fainali na ule wa kumsaka mshindi wa tatu ikifanyika siku ya jumamaosi Desemba 5.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.