Jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita Alphonce Mawazo ukiwasili katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza. |
WAKATI HUO HUO.
Polisi mkoani Geita wanawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Mwenyekiti wa Chadema mkoani humo, Alphonce Mawazo (pichani).
Mawazo alishambuliwa juzi na watu wasiojulikana katika Kijiji cha Katoro, Geita muda mfupi baada ya kutoka kwenye kikao cha ndani cha ya maandalizi ya uchaguzi wa diwani wa Kata ya Ludete.
Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema watu hao wamekatwa kwa kuhusishwa na mauaji hayo yaliyofanyika juzi saa 12.45 mchana katika eneo la Ludete A.
Mwabulambo alisema siku ya tukio kabla ya mauaji hayo, wafuasi wa Chadema walikuwa na kikao cha ndani katika eneo la Ludete B huku wenzao wa CCM wakiwa na kikao eneo la Ludete A.
“Hawa wa Chadema walivyokuwa kwenye kikao aliingia mtu akamnong’oneza Mawazo, hali iliyozua hofu kwa wengine na walipotoka nje wakakutana na kundi la watu na hapo kukazuka tafrani iliyosababisha watu wawili kujeruhiwa,” alisema.
Kamanda alidai kuwa haieleweki Mawazo alitokaje katika eneo walilokuwa wanafanyia kikao, lakini baada ya muda mfupi, wafuasi wa Chadema walipata taarifa kuwa yupo eneo la Ludete A karibu na ofisi za CCM na hali yake ni mbaya.
Alisema inadaiwa watu waliompiga Mawazo ni kundi la watu zaidi ya 10 na polisi wanaendelea na uchunguzi kuwabaini watu hao na chanzo cha mauaji hayo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.