ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 10, 2015

MIKOPO YA WANAFUNZI 40,836 tayari- HESLB


Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa

Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Omega Ngole 
By Vicky Kimaro, Mwananchi
Dar es Salaam. Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), imewapangia mikopo wanafunzi 40,836 baada ya kukidhi vigezo vyake.
Taarifa hiyo ya HELSB imetolewa siku moja baada ya Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) kuipa bodi hiyo saa 72 itoe majibu kwanini asilimia 82 ya wanafunzi wa vyuo vikuu wamekosa mkopo kwa mwaka huu wa masomo wa 2015/16.
Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Omega Ngole alisema jana kuwa katika awamu ya kwanza, bodi hiyo ilitoa orodha ya waombaji 12,282 waliofanikiwa kupata mikopo.
Alisema katika awamu ya pili iliyotolewa jana, waombaji wengine 28,554 walipewa mikopo hiyo.
Ngole alisema majina ya waombaji waliofanikiwa kupata mikopo kutoka awamu zote mbili ikiwamo ya jana (Novemba 9), yanapatikana kupitia tovuti za www.olas.heslb.go.tz na www.heslb.go.tz.
“Lengo la bodi ni kuhakikisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza wenye sifa wanapata mikopo katika mwaka wa masomo 2015/2016,” alisema Ngole.
Hata hivyo, aliwasihi waombaji kuwa watulivu wakati mchakato wa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa ukiendelea.
Kauli ya HESLB imekuja huku kukiwa na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa bodi hiyo haitatoa mikopo kwa waombaji wapya kwa mwaka mpya wa masomo.
Juzi, Bavicha iliitishia kuhamasisha wanafunzi kufanya mgomo wa amani bila kuleta madhara ili kushinikiza kupata mikopo.
Baraza hilo la vijana iliitaka bodi ya mikopo itaje vigezo na sababu walizotumia kutoa mikopo kwa baadhi ya wanafunzi na wengine kuachwa.
Kwa mujibu wa Bavicha, asilimia 82 ya wanafunzi waliokosa mikopo ni sawa na zaidi ya wanafunzi 70,000 wanaopaswa kupata mikopo hiyo inayotolewa kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini. CHAANZO MWANANCHI.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.