…East African Melody, Cassim Mganga ndani ya
nyumba
Hatimaye albamu ya “Sura Surambi” iliyokuwa
ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa taarab, inazinduliwa Alhamisi hii
Novemba 26.
Albam hiyo kutoka kwao Mashauzi Classic,
itazinduliwa ndani ya ukumbi wa Mango Garden Kinondoni huku kundi kongwe la
taarab East African Melody, likizindikiza tukio hilo kubwa.
Mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Mashauzi
ameuambia mtandao huu kuwa albam ya “Sura Surambi” inaundwa na nyimbo sita
kali.
Ni Alhamisi ya kihistoria ambayo Isha anaitaja
kuwa itapambwa na ratiba iliyokwenda shule itakayomwacha mshabiki apate uhondo
mwanzo mwisho.
Isha amezitaja nyimbo hizo kuwa ni pamoja na
“Sura Surambi” aliouimba yeye, “Kupendwa Bahati Yangu” uimbaji wake Abdumalick
Shaaban, na “Mjinga Mpe Cheo” wa Zubeida Malick.
Nyimbo nyingine alizozitaja Isha ni “Pendo la
Ukakasi” wa Saida Ramadhan, “Ubaya Haulipizwi” ulioimbwa na Asia Mzinga na
“Mapenzi Yamenivuruga” mwimbaji akiwa ni Naima Mohamed. Nyimbo zote hizo sita
zimetungwa na Isha Mashauzi.
Mbali na Melody, mkali wa tungo za mapenzi wa
muziki wa kizazi kipya Cassim Mganga naye pia atasindikiza uzinduzi huo wa
“Sura Surambi” ndani ya Mango Garden Alhamisi hii.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.