ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, October 11, 2015

SKYLIGHT BAND KUKINUKISHA LEO KIOTA CHA ESCAPE ONE KATIKA SUNDAY BONANZA, USIKOSE!

Sam Mapenzi ambaye ni mmoja wa waimbaji wa Skylight akitoa burudani na kusindikizwa na waimbaji wenzake.
Waimbaji wapya wa Bendi ya Skylight ambao ni Suzy (kushoto) akiimba pamoja na Sarah (kulia) mbele ya mashabiki wao (hawapo pichani)
Mwimbaji wa bendi ya Skylight Natasha akiimba moja ya nyimbo zinazobamba hapa nchini uku akisindikizwa vizuri na Mwimbaji mwenzake Ashura Kitenge (kushoto)
Mwimbaji mpya wa Bendi ya Skylight, Suzy akitoa burudani ya nguvu ndani ya Kiota ch Escape One Mikocheni jumapili iliyopita
Ilikuwa noma sana siku ya Jumapili iliyopita maana ilikuwa sio ya kupitwa basi mchuke na ndugu, jamaa au rafiki yako leo Jumapili uje kuona vitu vitamu kutoka kwenye Bendi ya Skylight ndani ya kiota cha Escape One, Mikocheni jijini Dar.
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiimba huku mashabiki wa bendi hiyo wakiserebuka kwa furaha na leo sio ya kukosa njoo na mwenzako uje kuona vitu vipya katika anga za muziki wa Live Escape One.
Kasongo Junior wa Skylight band akiimba kwa hisia kali mbele ya mashabiki i wa bendi hiyo (hawapo pichani) waliofika kwenye kiota cha Escape One Mikocheni.
Waimbaji wa bendi ya Skylight wakiima kwa pamoja moja ya nyimbo ya Bendi hiyo wa kwanza kushoto ni Joniko Flower, katikati ni Sony Masamba na kulia ni Sam Mapenzi
Mwimbaji wa Bendi ya Skylight, Kasongo Junior (kulia) akiimba sambamba na Suzy.
Rapa mkongwe katika muziki wa Live Joniko Flower(wa kwanza kushoto) akiimba moja ya sebebene uku akisindikizwa na wananamziki wenzake katikati ni Sony Masamba
Mwimbaji wa bendi ya Skylight, Sam Mapenzi(kulia) akiimba sambamba na mpiga gitaa Alen Kisso walipokuwa wakiwakonga nyoyo mashabiki wao ndani ya kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar jumapili iliyopita
Wapenzi wa Bendi ya bendi ya Skylight wakiendelea kuziruka ngoma zilizokuwa zikiimbwa na bendi hiyo jumapili iliyopita katika kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.