TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Arusha Mjini kimesikitishwa na kuhuzunishwa na kifo cha mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, Ndugu Estomih Jonas Mallah ambaye alipata kuwa Mwanachama na Diwani Kata ya Kimandolu kupitia CHADEMA katika Wilaya hii.
Tumepokea kwa masikitiko makubwa na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Ndugu Estomih Jonas Mallah ambaye tumejulishwa kuwa aliaga dunia usiku wa kuamkia Ijumaa, Oktoba 9, 2015, katika Hospitali ya Rufaa- KCMC, Mkoani Kilimanjaro. Ni dhahiri Wanademokrasia tumeondokewa na mtu muhimu katika kipindi muhimu.
Tunatuma salamu za dhati kuomboleza kifo cha Ndugu yetu Estomihi Jonas Mallah kwa familia, Viongozi na Wanachama wa chama cha ACT- Wazalendo.
Kwa pamoja tunamwomba Mungu mwenyeenzi, Mwingi wa Rehema, atupe subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya Marehemu Estomih Jonas Mallah. Amen
Lewis Emmanuel Kopwe
Kaimu Mwenyekiti
Wilaya ya Arusha Mjini
10/09/2015
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.