Akitangaza uamuzi huo mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Bw. Lubuva ametolea mfano wa kusimamishwa kwa uchaguzi Tz Bara wa mwaka 2005 baada ya mgombea mwenza NCCR Mageuzi Ali Omar Juma kufariki dunia ambapo uchaguzi Zanzibar uliendelea kama kawaida.
Ifuatayo ni sehemu ya barua toka Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC)...
Akiongea baada ya kutolewa tangazo hilo, Katibu Mkuu wa CUF na ambaye alikuwa mgombea wa kiti cha urais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema hatambui uamuzi huo kwani mwenyekiti wa tume hana mamlaka ya kuamua bila kuwashirikisha makamishina.
Maalif Seif amesema wanawasiliana na taasisi za kimataifa na msaada juu ya jambo hilo.
Pia baada ya kutolewa kwa uamuzi huo na ZEC, Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wamekutana na waandishi wa habari na kusema kuwa hawatakubali matokeo yanayoendelea kutolewa na NEC.
Hata hivyo, CCM kupitia Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za chama hicho, January Makamba amesema ni vema wanasiasa wakawana utaratibu wa kupokea na kukubali matokeo na kwamba anashangazwa na Ukawa kuanza kuonesha dalili za kuyakataa matokeo.
Akitolea ufafanuzi kuhusu uamuzi huo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema hilo halitaadhiri uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Muungano.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.