ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 5, 2015

MKURUGENZI TAKUKURU ASEMA MIAKA 10 YA JK IMEPAMBANA NA RUSHWA KWA KIASI KIKUBWA


Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru nchini, Dkt. Edward Hoseah akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya ambapo amesema kuwa Taasisi  hiyo imeweza kufanikiwa  kupambana na rushwa kwa kiasi kikubwa  ambapo jumla  kesi kubwa za rushwa 1,993 kuanzia mwaka 2004-2015 zimeweza kufunguliwa ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia 81 ikilinganishwa na kesi 384 zilizokuwepo miaka 10 ilioyopita (1995-2004).

 Amesema ,ongezeko hilo la kesi kubwa limetokana na jitihada za Taasisi hiyo katika kupambana na kuzuia rushwa nchini hasa katika kipindi cha serikali ya awamu ya nne, chini ya rais Jakaya Kikwete.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akitoa salama za mkoa wa mbeya katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Takukuru Mkoa wa Mbeya .
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mbeya xavery Mhyella akatoa taarifa ya Takukuru Mkoa wa Mbeya mbele ya Mgeni rasmi katika hafla hiyo ambayo imehudhuriwa na  Mkurugenzi wa Mkuu  Takukuru  nchini Dkt, Edward Hosea Octobar 5 mwaka huu..Picha na Emanuel Madafa ,Jamiimojablog Mbeya 
Mkaguzi Mkuu wa Kanda Takukuru Ndugu Joice Shundi akizungumza katika hafla hiyo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Wende wakitoa burudani za ngoma za asili katika uzinduzi huo wa jengo la ofisi mpya ya Takukuru Mkoa wa Mbeya .

Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa dini waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa jengo zilizopo eneo la forest ya zamani karibu na Mahakama kuu jijini Mbeya.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.