Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&M, Baseev Mohamed (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.milioni 20, Mkuu wa Idara ya Biashara wa benki hiyo, Svikanth T, kwa niaba ya mteja wa benki hiyo, Jumanne Francis Mchenje wa Tarime mkoani Mara anayeishi jijini Mwanza aliyejinyakulia kitita hicho cha fedha baada ya kushinda bahati nasibu ya kwanza inayoendeshwa na benki hiyo kwa ajili ya kuongeza wateja wapya iliyofanyika Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja Masoko, Ruheen Kaba.
Bahati nasibu hiyo iliyowashirikisha wateja wa benki hiyo ikichezwa.
Namba iliyoshinda ikihakikiwa. Wa pili kushoto ni Mjumbe kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Jehud Ngolo.
Maofisa wa benki hiyo wakisubiri kuanza kuchezwa kwa baahati nasibu hiyo.
Hapa aliyechaguliwa kuchagua namba akifungwa kitambaa.
Mashine ikichangany'a namba za kushiriki bahati nasibu hiyo.
Bahati nasibu hiyo ikichezwa.
Kitambulisho cha mshindi wa bahati nasibu hiyo, Jumanne Francis Mchenje.
Na Dotto Mwaibale
BENKI ya I&M Ltd imeanzisha mchezo wa bahati nasibu kwa wateja wapya wanaojiunga kwenye benki hiyo kwa lengo la kuvutia wataje wao.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Baseer Mohamed alisema shindano la kwanza lilifanyika jana ambapo Jumanne Francis Mchenje kutoka Tarime mkoa wa Mara aliibuka kuwa mshindi.
Alisema Jumanne alijishindia Million 20 kwa kufungua akaunti katika benki hiyo na kuweka kiasi kidogo cha pesa kwenye akaunti yake.
"Jinsi ya kushiriki bahati nasibu hii ni kufungua akaunti ya benki yetu kisha kuweka kiasi chochote kwenye akauti yako ndipo tunakuingiza kwenye droo ya kujishindia million 20,"alisema Mohamed.
Alisema watakuwa wakifanya mashindano kama hayo kila wiki ili kuonyesha utamaduni mzuri kwa wataje wao kwani benki hiyo ni makini.
Pia aliwataka wananchi kufungua akaunti zao katika kipindi hiki cha bahati nasibu ili kujishindia kitita hicho cha million 20 kila. wiki.
"Benki hii ni kwa ajili ya Watanzania wote hivyo ni vyema mkajitokeza kwa wingi kufungua akaunti zenu na kufurahia huduma zinazo tolewa na benki yetu,"alisema Mohamed.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.