ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 12, 2015

LOWASSA AZIDI KUKOMALIA SERA YA ELIMU BURE.

Mgombea urais kupitia CHADEMA na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Edward Lowassa leo ameendelea na kampeni zake katika mkoa wa Mwanza.
Lowassa amepokewa na ummati mkubwa katika viwanja vya Furahisha Kirumba jijini Mwanza.
Engo kutoka juu ghorofani.
Mgombea urais kupitia CHADEMA na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Edward Lowassa leo ameendelea na kampeni zake katika mkoa wa Mwanza. Akizungumza katika mkutano huo Lowassa ameendelea kusisitiza juu ya sera ya kutoa elimu bure kuanzia ngazi ya awali hadi chuo kikuu.
Furahisha Kirumba na umma uliojitokeza kusikiliza sera.
Mwenyekiti Mwenza wa vyama vya ukawa James Mbatia amewataka watanzania kutokubali kuyumbishwa kwa hoja ya afya kwa mgombea huyo wa urais. 
MSIKILIZE HAPA.

Mwanza.
Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katikati ya umma akiamasisha.
Wananchi wa mkoa wa Mwanza katika  kusanyiko la kampeni za Mgombea urais kupitia CHADEMA na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Edward Lowassa zilizofanyika leo katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza. Aliyekuwa waziri Mkuu wa zamani wa Serikali ya awamu ya tatu Fredrick Sumayi amesema mfumo wa vyama vingi ni demokrasia hivyochama chochote chenye sera zenye  kukubalika kwa wananchi kina nafasi ya kupata ridhaa ya kuwatumikia wananchi  MSIKILIZE SUMAYI 
Mgombea nafasi ya ubunge jimbo la Ilemela Higness Kiwia (mbunge mwenyeji) alipata nafasi ya kuomba ridhaa ya wananchi kwa kipindi kingine.
Mitaa ya jirani na eneo la mkutano.
Watu na watu wao, siasa na wananchi.
Ni muda wa kusambaa mara baada ya mkutano kumalizika.
Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.