ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 16, 2015

JUHUDI ZA KUINUA ELIMU ZAFANYIKA WILAYANI KAHAMA

Na Emmanuel Mlelekwa,
Oktoba 16,2015.
KAHAMA

Ikiwa Serikali ipo kwenye mkakati wa kuinua kiwango cha Elimu nchini kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa sasa(BRN) shule ya Msingi Korogwe iliyopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeamua kutekeleza Mpango huo kwa kutoa huduma ya Chakula kwa Wanafunzi shuleni hapo.

Akizungumza kwa  niaba ya Mkuu wa Shule hiyo mwalimu wa Taaluma Josepha Jamal amesema uongozi mpango huo unatarajia kuanza Januari mwakani kwa kuwapatia chakula wanafunzi wote ili kuinua ari zao katika kujifunza.

Jamal amesema kuwa uongozi wa Shule hiyo tayari umeshafanya utekelezaji wa huduma ya Chakula kwa wanafunzi waliomaliza darasa la 7 mwaka huu na uji majira ya asubuhi katika madarasa mengine hivyo wanatarajia kutekeleza kwa shule nzima.

Hata hivyo ameomba serikali na wazazi kutoa ushirikiano katika kutekeleza hilo kwani moja wapo ya sababu inayopelekea wanafunzi
kutofanya vizuri ni njaa wakati wa vipindi hivyo kuwepo kwa mpango huo kutawafanya wanafunzi kujifunza kwa ufanisi zaidi tofauti na sasa.

Hayo yanakuja baada ya jitihada ya UWEZO chini ya asasi ya kiraia ya TWAWEZA kupitia shirika la REITCHET Foundation lililopo wilayani Kahama kufanya dodoso la uwezo wa wanafunzi katika kujifunza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.