Marehemu Deo Filikunjombe. |
Mgombea Ubunge Tanzania Deo Filikunjombe afariki.
Deo Filikunjombe aliyekuwa anatetea jimbo lake la LUDEWA kwa tiketi ya CCM anakuwa mbunge wa sita kupoteza maisha katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu na hivyo utalazimu pia uchaguzi wa ubunge kuahiriswa kwenye jimbo hilo.
Kamishna wa operesheni na mafunzo wa Jeshi la polisi, nchini Tanzania Paul Chagonja amethibitisha kutokea kwa ajali ya helikopta Nnamba 5YDKK katika eneo la pori la selou kwenye kijiji cha Mtende mkoani Morogoro iliyosabaaisha vifo vya watu wanne akiwemo mgombea wa ubunge jimbo la Njombe Deo Filikunjombe.
Akizungumza na Sauti ya Amerika kwa njia ya simu tokea eneo la tukio kamishna Chagonja amesema maiti nyingine iliyotambulika ni ya rubani wa helikopta hiyo William Slaa huku abiria wengine wawili ambao ni wanaume wakiwa bado hawajatambulika.
Amesema hivi sasa vikosi vya uokoaji vinafanya jitihada za kuitoa miili ya marehemu katika eneo la tuko kwa ajili ya uchunguzi huku akisita kuelezea chanzo cha ajali hiyo ya helikopta..
**Mara baada ya habari za uhakika kupatikana hivi ndivyo Mstahiki Meya wa Ilala Mhe. Jerry Silaa aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa instagram.
Taarifa za kuanguka kwa helikopta iliyopoteza uhai wa deo Filikunjombe aliyekuwa mbunge machachari na makamu mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali katika bunge lililopita zilianza kusambaa jana jioni katika mitandao mbalimbali ya kijamii na hatimaye majira ya mchana Ijumaa leo ndio ikathibitika kwamba watu wote waliokuwemo kwenye helikopta hiyo wamefariki dunia
Kamishna Chagonja amesema polisi na taasisi nyingine ikiwemo mamlaka ya usalama wa anga imeanza uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo ya helikopta ambayo inadaiwa ilikuwa imekodiwa na Marehemu Deo Filikunjombe
Deo Filikunjombe aliyekuwa anatetea jimbo lake la LUDEWA kwa tiketi ya CCM anakuwa mbunge wa sita kupoteza maisha katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu na hivyo utalazimu pia uchaguzi wa ubunge kuahiriswa kwenye jimbo hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.