![]() |
Ofa hii ya kipekee itawawezesha wateja wa Airtel kufurahia kuperusi internet bila kikomo wakati wa usiku kila siku. Huduma ya internet imeendelea kuileta dunia karibu, Kupitia huduma za internet dunia imeletwa karibu na kuwa kijiji kimoja.
Takribani asilimia 42.4 ya watu duniani wanatumia huduma ya intaneti, kati yao bilioni 2 wanatoka katika nchi zinazoendelea, wakati milion 89 wanatoka katika nchi ambazo hazijaendelea. Kwa wastani asilimia 34 ya wakazi katika nchi zinazoendelea wameunganishwa na huduma za intaneti (kumb. ITU).
Katika shughuli zetu za kila siku ,wakati wa mchana ni vigumu kupata muda wa kutumia intaneti kwa mambo yetu binafisi, Ofa hii ya yatosha nights itatupatia fulsa ya kutumia huduma ya inanet na kuunganishwa na jamii kwa urahisi zaidi muda jioni.alisema Gaurav Dhingra Mkuu wa huduma za intaneti. “leo tunawawezesha wateja kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo kuangalia sinema, mpira, kutuma picha na video kwa marafiki na wapendwa wao, kupata taarifa za habari mbalimbali zinazotokea duniani na nchni bila kujali muda na kiasi cha kifurushi cha data kitakachotumika.
Kwa shilingi 600 kuanzia saa 6 usiku mpaka saa 12 asubuhi tunawawezesha watanzania nchi nzima kupata intenati bila kikomo kupitia Yatosha Nyts”. Dhingra aliongeza kwa kusema , wateja wanaweza kununua kifurushi hiki cha usiku wakati wowote , ili kujiunga mteja anatakiwa kupiga *149*99# na kuunganishwa kwenye menu ya Airtel Yatosha , kisha kuchagua 4 ili kupata Yatosha Nyts and kisha kufata maelekezo.
Airtel Tanzania chini ya huduma ya Yatosha wiki iliyopita ilizindua ofa ya Yatosha Nyts inayompatia mteja uhuru wa kuongea na familia, marafiki, wapendwa na wafanyabishara wenzao bila kikomo kwa shilingi 300. Ofa hii ya intaneti bila kikomo ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel ya kuleta mawasiliano bora na kuwawezesha watanzania nchini nzima kutumia huduma za intaneti
Tupe maoni yako




0 comments:
Post a Comment