Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (PICHA MAKTABA) |
Na Kahema Emanuel,Mbeya
Wito umetolewa kwa Waratibu wa uchaguzi wa mikoa ,wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na
maafisa uchaguzi wa halmashauri mikoa ya kanda za juu kusini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa waledi na
kwa uadilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa ua mgombea .
Kauli hiyo
imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro wakati akifungua mafunzo
ya wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi halmashauri
ambao ni wakurugenzi wa halmashauri na maafisa uchaguzi katika mikoa ya Iringa na Mbeya.
Amesema ili
zoezi hilo la uchaguzi liende vizuri na lisighubikwe na vurugu nivema
wasimamizi hao wakatumia waledi wao na udilifu bila kuwa na upendeleo wa chama
chochote cha siasa au mgombea yoyote ili kuepuka hali hiyo.
Amesema mara
baada ya kupatiwa mafunzo hayo nivema wakaendelea kutumia muda wao wa ziada
kusoma na kupitia vitabu vya maelekezo
waliyopatiwa kwa kutumia kanuni na maadili ya uchaguzi ili kuimarisha uelewa
zaidi kuhusu wajibu na majukumu yao katika zoezi hili la uchaguzi mkuu mwezi
octobar.
Amesema
pamoja na majukumu mengine waliyonayo pia wametakiwa kutoa kipaumbele katika
kutekeleza zoezi hili la kitaifa kwa ufanisi zaidi na kwa muda uliopangwa kwani
uchaguzi huu utafanyika kwa siku moja tu kwa kila baada ya miaka mitano.
Aidha
amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetekeleza jukumu lake katika hatua ya
mafunzo na maandalizi ya vifaa na rasilimali nyingine hivyo wao kama wasimamizi
wanatakiwa kutekeleza wajibu wao katika ngazi zote kwa mujibu wa taratibu
zilizopangwa na Tume.
Katika
semina hiyo wasimamizi hao watajifunza wajibu wa wasimamizi wa vituo vya
kupigia kura ,uwendeshaji wa zoezi la
upigaji kura vituoni sanjali na
uendeshaji wa zoezi la kuhesabu kura,kujumlisha kura na kutanganza matokeo ya
uchaguzi.
Afisa Uchaguzi Kanda ya Nyanda za juu kusini -Tume Ndugu Jane Tungu akizungumza katika semina hiyo. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.