VICTOR MASANGU, KISARAWE PWANI
SHIRIKA la kimaendeleo linalojishughulisha na kutoa misaada kwa binadamu Plan International limebaini kuwepo kwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wadogo kulawitiwa hali ambayo imeelezwa inachangiwa kwa kiasi kikubwa kutokana familia zao kutengana au ndoa kuvunjika na kupelekea watoto wengi kukosa malezi bora na kuishi katika mazingira magumu.
Hayo yamebainika baada ya shirika la Plan international kufanya ziara ya kutembelea katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuweza kubaini changamoto mbali mbali zinazowakabili watoto hao pamoja na kuweka mikakati madhubuti yenye lengo la kuwalindana kuwapatia haki zao za msingi.
Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa mradi Violence Against Children (VAC) ulianzisha kwa ajili ya kupinga vitendo vya ukatili kwa watoto kutoka shirika la Plan international Wilaya ya Kisarawe Neema Dainel amesema kwamba kwa sasa baada ya kufanya uchunguzi wamegundua baada ya wazazi kutengana watoto hao wanaishi katika mazingira magumu kutokana na kulelewa na babu au bibi huku wazazi wao wakiwa hawapo.
NEEMA MRATIBU WA MRADI
Aidha Mratibu huyo amebainisha kwamba kwa sasa kesi za ukatili dhidi ya watoto zimeongezeka kutoka kesi 10 kwa mwaka 2014 hadi kufikia kesi 59 kwa kipindi cha mwaka 2015 ambazo tayari zimekwisha ripotiwa na kufanyiwa uchunguzi na kwamba ongezeko hilo limetokana na elimu waliyoitoa kwa jamii ya kuhakikisha inawafichua watu wanaohusika na vitendo hivyo vya ukatili bila ya uwoga.
MRATIBU
Kwa upande wake Meneja wa mradi wa Kisarawe Unit William Mtukananje akusita kulitolea ufafanua sababu kubwa amabzo zinachangia kuongezeka kwa kesi za ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto hao.
MENEJA WILLIAM
Mwandili Longi yeye ni Afisa ustawi wa jamii Wilaya ya Kisarawe anafafanua ni hatua gani ambazo wanazichukua endapo wakimbaini mtu mwenye kosa la kuwafanyia vitendo vya ukatili watoto.
CUE IN.. 4 LONGI
Mradi huo unaojulikana kwa jina la Violence Against Children (VAC ambao ulianzishwa mwaka 2014 ambapo katika Mkoa wa Pwani umeshaanza kufanya kazi katika Wilaya mbili za Kisarawe pamoja na Wilaya ya Kibaha kwa lengo la kuweza kupinga ukatili dhidi ya watoto pamoja na kuanzisha mabaraza mbali mbali ,katika ngazi zote za vijiji, kata na Wilaya lengo ikiwa kuielimisha jamii kuhusu haki za mtoto pamoja na ulinzi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.