WAZAZI na walezi hapa nchini wametakiwa kuachana na mila zilizopitwa na wakati kwa kuwaozesha watoto wao mapema hususan wa kike wakiwa katika umri mdogo na kupelekea baadhi yao kukatisha masomo yao na badala yake wawe na mawazo chanya ya kuwasaidia katika kuwalinda na kuwapatia haki zao za msingi katika elimu.
Kauli hiyo imetolewa na mwanafunzi mmoja anayesoma kwa sasa kidato cha tatu ambaye jina lake linahifadhiwa kutokana na kulinda haki za watoto wakati wa ziara ya siku mbili Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani iliyofanywa na shirikika la kimaendeleo linalojishughulisha na kutoa misaada kwa binadamu Plan International kwa lengo la kubaini changamoto zinazowakabili watoto.
Mwanafunzi huyo akizungumza kwa majonzi na waandishi wa habari pamoja na watendaji wa halmashauri ya Kisarawe pamoja na watumishi wa Plan international amesema kwamba amesikiteshwa sana kuona wazazi wake wanamkatisha masomo yake na kumwozesha kwa nguvu bila lidhaa yake kwa mwanaume.
Aidha binti huyo amebainisha kuwa baada ya mwaka 2014 mwanzoni kumkatalia baba yake mzazi kuolewa ndipo mazi wake alipoamua kutumia njia nyingine ya kumdang’anya anamtafutia uhamisho wa kwenda kusomea shule nyingine iliyopo Wilayani Mkuranga kumbe alikuwa tayari amemtafutia mwanaume kwa nguvu kwa lengo la kumwozesha mwanae wa kumzaa.
Kwa upande wake Afisa ustawi wa Jamii Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani amethibitisha kutokea kwa taarifa za tukio hilo la mwanafunzi na kwamba wamempokea na kumpatia msaada wa hali na mali ikiwemo kumpatia mahitaji muhimu na kumpeleka shule ambapo kwa sas anaendelea na masomo.
Kwa upande wake mmoja wa mjumbe wa kamati ya ulinzi ya mtoto Wilaya ya Kisarawe Saimon Mpunga akizungumza kwa niaba ya wajumbe wenzake amesema kwamba kuja haja ya kuwafichua wazazi wenye tabia kama hizo na kuongeza kuwa baada ya mradi huo wa wa kupinga ukatili dhidi ya watoto kuanziashwa na Plan International jamii imeweza kuvunja ukimya.
Jembe Fm iliweza kupata fursa ya kuzungumza na mama mlezi ambaye anamlea mwanafuzni huyo kwa sasa aliyejitambulisha kwa jina la Veronica Kilango na hapa alikuwa na haya ya kusema kuhusiana na msicha huyo.
Kuanzishwa kwa Mradi huo wa Plan International wa kupinga ukatili dhidi ya watoto umeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa na kufanikiwa kumpata na kumsaidia mwanafunzi huyo ambaye aliozeshwa na baba yake mzazi kwa mwanaume mwenye umri wa mika (30) kwa ng’ombe 150.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.