Mgombea ubunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza jambo na wananchi waliofika kushuhudia sherehe za kufanyika kwa uzinduzi wa tawi la Young Quality. |
Mmoja wa wakeleketwa na mwanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) Mufindii Msagahaa akizungumza na wananchi katika moja ya mikutano ya mgombea mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvesetry Koka |
Mmoja wa viongozi wa tawi hilo la Young Quality akisoma risala kwa mgombea ubunge jimbo la Kibaha mjini Silvesetry Koka mara baada ya kufanyika rasmi jwa ufunguzi wa tawi hilo. |
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
VIJANA hapa nchini wametakiwa kuachana na makundi ya kihuni na kukaa vijiweni bila kazi yoyote na badala yake sasa wahakikishe wanajikita zaidi katika shughuli mbali mbali za ujasiliamali ili kuweza kuondokana na hali ya kuwa tegemezi kila kukicha na kupambana na janga la umasikini.
Kauli hiyo imetolewa na Mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka alipokuwa akizungumza na vijana wakati wa hafla fupo ya ufunguzi wa tawi jipya la CCM, katika kata ya maili lililopewa jina la Young Quality.
Koka alisema kwamba amebaini kwamba baadhi ya vijana wanalalamika kutokuwa na ajira kumbe wao wenyewe wamekuwa hawataki kujishughulisha katika kazi mbali mbali, hivyo amewaomba endapo wakijiunga katika amkundi ya ujasiliamali atahakikisha anakuwa nao bega kwa bega katika kuwasaidia kwa hali na mali mitaji kwa ajili kuanzisha bishara.
“Kwa kweli mimi kwa upnde wangu sipendi kuona vijana wangu mnapata shida wakati mimi nipo hasa kwauapande wa vijana wa jimbo langu la kibaha mjini lakini kitu kikubwa mimi nipo pamoja nanyi ila kitu kikubwa cha msingi ni kuwa pamoja katika vikundi mimi nitawawezesha ili kuondokana na kuwa tegemezi,”alisema Koka.
Aidha Mgombea huyo alisema kuwa aina imani vijana hao katika siku za mbeleni wakijiwekea malengo ya dhati na kuhakikisha wanashirikiana kwa udi na uvumba wataweza kupiga hatua kubwa katika kuleta ukombozi mkubwa wa kimaendeleoa katika Jimbo la Kibaha Mjini.
Koka alibainisha kuwa anapenda kuona vijana wa jimbo lake kuanzia ngazi zote za mtaa hadi ngazi ya Wilaya wanafanikiwa kwa kiasi kikubwa kupitia biahsra zao ambazo wamekuwa wakizifanya na sio kukaa tu vijiweni bila ya kuwa na malengo yoyote yale katika biashara zao.
Katika hatua nyingine aliwakumnusha vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika occtoba 25 mwaka huu bila ya kutishwa na mtu yoyote kwani ulizni umeimalishwa na serikali ya chama cha mapinduzi ili uchaguzi uwe wa amani na utulivu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.