ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 25, 2015

Dr. NGELELA (CHADEMA) AKILI KUSHINDWA NA CCM JIMBO LA ULYANKULU PAMKA WAGOMBEA WANGEUNGANA IKIWEMO ACT-Wazalendo

Na PETER FABIAN, KALIUA.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo jipya la Uchaguzi la Ulyankulu kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr Deus Ngelela amewaomba wananchi wa jimbo hilo kufanya mabadiliko kwa kuchaguwa wagombea vyama vinavyounda UKAWA ili kuwatetea na kuwaletea maendeleo.

Dr Ngelela akizungumza na wananchi katika moja ya Kata ya Kona nne jimboni humo, aliwaeleza wananchi kwamba muda wa kufanya mabadiliko ni mwaka huu na wakishindwa kufanya uamuzi wa kukiondoa madarakani Chama Cha Mapinduzi basi watambue awataweza tena kufanya hivyo na itwachukua miaka mingine 20 ijayo kupata mgombea Urais kama Lowassa na ubunge.

“Nawaombeni mumuchague mgombea wa CHADEMA kwa nafasi ya Urais Edward Lowassa ili awaletee maendeleo ya kweli na mimi mnichague kuwa Mbunge wenu lakini pia msisahau kuwachagua madiwani wetu tufanye mbadiliko ya maendeleo na si CCM iliyoshindwa,”alisema.

Katika mukutano huo ambao ulihudhuriwa na wananchi wachache kutokana na mwamuko mdogo wa wananchi wa maeneo hayo wengi wao kutoka maeneo mbalimbali ya miji ya Tabora, Kaliua, Mpanda, Kahama na Ulyankulu kujishughulisha na biashara, kilimo na ufugaji.

Dr Ngelela akijinadi na kuomba kura kwa wananchi hao aliwashangaza na kuibuwa kicheko pale aliposema anawania Ubunge lakini anajua atashindwa na John Kadutu (CCM) kutokana na Chama chake kuwa na ujanja na mbinu ya kuiba kura zenu mtakazonipigia katika uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka huu.

“Nijipe Moyo lakini natambua kuwa huyo Kadutu atanishinda lazima nikiri anaonekana kujiamini kunishinda lakini niwaombe msikate tamaa jitokezeni kunipigia kura mimi na Lowassa kwani Dr Ngelela niko kama mbwa wenu mnayemfungia mchana na usiku mnamwachia kuwalinda awalinde hivyo komaeno makamanda inawezekana kikaeleweka na tukachukua jimbo hili CHADEMA,”alisisitiza.

Alisema kwamba wapo mgombea wengine mbali na Kadutu wa CCM pia mgombea mwingine ni Kayoka Nicholaus (ACT-Wazalendo) ambaye ametuharibia kwa kung’ang’ania kugombea na kusababisha mvutano wetu na huenda tukazigawana kura zetu jambo ambalo litampa mtelemuko Katudu kutushinda kilahisi ni vyema wangekubali kuniunga mkono mimi ili nimshinde kutoka na kukubalika kwa wananchi kuliko Nicholaus.

Baada ya mkutano huo uliozua mijadara ya hapa na pale kwa wananchi wa Kata ya Kona nne kuzua mabishano na kumjadili mgombea huyo huku baadhi yao wakiwa katika vikundi tofauti kudai kwamba Dr Ngelela ameshindwa kujikita kwenye sera, kutoa ahadi na kujenga ushawishi kwao ili kumchagua zaidi ya kumsema Kadutu na Nicholaus.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.