ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 21, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MPANGO WA KAZI WA KIMATAIFA NA KANUNI ZA SHERIA YA KUZUIA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizindua Mpangokazi wa Kimataifa na Kanuni za Sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa Binadamu, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika leo Agosti 21, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (kulia) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Kinemo Kihonamo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Mpangokazi wa Kimataifa na Kanuni za Sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa Binadamu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe, baada ya kuzindua rasmi Mpango kazi huo, kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Agosti 21, 2015. Picha na OMR
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua mpango kazi huo, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo Agosti 21, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo wakimsikiliza mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMR
Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo wakimsikiliza mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMR
Baadhi ya Wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo wakimsikiliza mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMR
Baadhi ya Wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo wakimsikiliza mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMR
Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo wakijisomea vipeperushi walivyogaiwa katika uzinduzi huo. Picha na OMR
Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo wakijisomea vipeperushi walivyogaiwa katika uzinduzi huo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo, baada ya uzinduzi. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo, baada ya uzinduzi. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo, baada ya uzinduzi. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo, baada ya uzinduzi. Picha na OMR

HOTUBA YA DKT. BILAL:-
HOTUBA YA MHE. DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL, MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWENYE UZINDUZI WA MPANGO KAZI WA KITAIFA NA KANUNI ZA SHERIA YA KUZUIA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU, KARIMJEE - DAR ES SALAAM,
 TAREHE 21 AGOSTI, 2015
  
Mhe. Mathias Chikawe
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi;

Ndugu Kinemo Kihomano
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu;

Waheshimiwa Makatibu Wakuu;

Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama;

Wakuu wa Idara na Vitengo;

Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na
Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu;

Waheshimiwa Mabalozi wa Nchi mbalimbali;

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM);

Wageni Waalikwa;

Ndugu Wanahabari;

Mabibi na Mabwana;


Habari za Asubuhi.

Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetujalia uzima na afya na kutuwezesha kukusanyika hapa siku ya leo katika tukio hili muhimu kwa ustawi wa nchi yetu  na haki za binadamu kwa ujumla.  Kwa namna ya pekee napenda kukushukuru wewe Mheshimiwa Mathias Chikawe, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kunipa heshima hii kubwa, kunialika kushiriki kwenye tukio hili la aina yake  la uzinduzi wa Mpango Kazi wa Kitaifa na Kanuni za Sheria ya Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu katika nchi yetu.  Vile vile, nachukua nafasi hii kukushuru Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati na Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadam,  kwa kuandaa Mpango Kazi na Kanuni za Kutekeleza Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu ambavyo tunatarajia kuvizindua muda mfupi ujao mahali hapa.

Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Leo tunazindua Mpango Kazi wa Kitaifa na Kanuni kwa ajili ya utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu  hapa nchini.  Lakini kabla ya uzinduzi huo, naomba niseme machache kuhusu tatizo hili. Usafirishaji haramu wa binadamu unahusisha upatikanaji, usafirishaji, uhamishaji, uhifadhi, utoaji au upokeaji wa mtu ambao hufanyika kwa njia zozote, zikiwemo zile za udanganyifu kupitia visingizio vya ajira za ndani au nje ya nchi, mafunzo, na lengo kuu likiwa ni madhumuni ya ukahaba, unyonyaji wa aina zote, ufanyishaji kazi lazimishi, utumwa, pronografia, au kufungwa na deni.  Usafirishaji Haramu wa Binadamu wakati mwingine unaitwa Utumwa.

Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Tafiti zilizopo zinaonesha kuwa zaidi ya watu 700,000 husafirishwa kutoka bara moja kwenda lingine au nchi moja kwenda nyingine kwa lengo la kutumikishwa katika migodi, mashamba ya kilimo na kazi za ndani.  Umoja wa Nchi za Ulaya umeripoti matukio mengi ya wahanga wa usafirishaji haramu wa binadamu kutoka katika mataifa 95 duniani likiwemo Bara la Afrika ambapo husafirishwa kwa lengo la kutumikishwa.  Inaripotiwa kuwa Tanzania nayo imeathirika na biashara hii ya usafirishaji haramu wa binadamu.  wanaume, wanawake  na watoto wamekuwa wakisafirishwa kutoka vijijini kwa lengo la kwenda kutumikishwa au kufanyishwa kazi mijini.  Taarifa zinaonesha pia Watanzania wamekuwa wakisafirishwa kupelekwa nje ya nchi hususan Mashariki ya mbali kwa lengo la kutumikishwa. Inasemekana kuwa Tanzania inatumika kama njia ya kupitisha wahanga wa biashara hii kutoka nchi moja kwenda nyingine.  Kutokana na kuwepo  matukio kadhaa ya kukamatwa kwa wageni ambao ni wahanga wa biashara hii, ni dalili kuwa Tanzania inapokea watu kutoka mataifa mengine kwa lengo la kuja kutumikishwa hapa nchini.

Ndugu Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Kwa upande wa Serikali katika kupambana na tatizo hili imeridhia mikataba ya Kimataifa na kutunga Sheria ya Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu Na. 6 ya mwaka 2008.  Napenda kuchukua fursa hii kuihakikishia jamii yetu na jumuiya ya kimataifa kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ina dhamira ya dhati  kuhakikisha kuwa tatizo hili linatokomezwa. 

Ndugu zetu washirika wa maendeleo na mabalozi mliopo hapa tunawapeni Mpango kazi wetu wa Kitaifa wa kupambana na tatizo hili.  Ombi langu kwenu uangalieni ili muone ni eneo lipi mnaweza kuunga mkono Serikali katika kuutekeleza.

Mheshimiwa Waziri;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Nimalizie hotuba yangu kwa kuwashukuru tena  kunialika katika uzinduzi huu. Vile vile napenda kutumia fursa hii kushukuru Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) kwa kazi nzuri ya ushauri wa kitaalam wanaoutoa kwa Kamati na Sekretariati ya Kitaifa katika kupambana na tatizo hili hapa nchini.  Kwa upande wenu wanahabari, mnalo jukumu kubwa la kuielimisha jamii juu ya uhalifu huu, athari zake na namna ya kukabiliana nalo. Tumieni vema kalamu zenu kusaidia katika mapambano haya.

Baada ya kusema hayo, kwa heshima kubwa na taadhima  napenda kutamka kwamba;  Mpango Kazi wa Kitaifa na Kanuni za Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu,  umezinduliwa rasmi.

 Asanteni sana kwa kunisikiliza.  

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.