Na mwandishi wetu
Wateja na watanzania wanaopenda soka kwa ujumla watapata fursa ya kufaidi mechi zote za ligi ya Ujerumani almaarufu kama ‘Bundesliga’ kupitia ving’amuzi vyao vya StarTimes.
Hayo yalibainishwa na uongozi wa Kampuni ya StarTimes Tanzania wakati wa hafla fupi ya kutangaza kuonyeshwa kwa ligi hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika makao yake jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi huo Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Michezo, Vijana na Utamaduni, Leonard Thadeo alisema kuwa Bundesliga ni ligi maarufu na inayopendwa duniani na anaipongeza kampuni ya kitanzania kwa mara ya kwanza kufanikiwa kupata hakimiliki za kuionyesha.
“Ni hatua kubwa waliyoipiga StarTimes kwa kufanikiwa kuionyesha ligi hii kupitia ving’amuzi vyao. Nina imani kubwa kuwa watanzania wengi wanaopenda soka watafurahia zaidi kwani nimeambiwa kuwa zaidi ya mechi 300 zitaonyeshwa moja kwa moja kupitia chaneli zao tofauti.” Alisema Thadeo
“Mbali na wapenda soka kufurahia ligi hii bali pia ni fursa kwa wachezaji wa kwetu nyumbani kuangalia ni kwa namna gani wenzao wanacheza soka la kulipwa. Kwani kupitia wenzetu ambao wamepiga hatua kubwa katika maendeleo ya soka yapo mengi ambayo tunaweza kujifunza na kuboresha ligi yetu,” alisema Thadeo.
“Napenda kutoa wito kwa watanzania kuendelea kuunga mkono juhudi za kampuni za kinyumbani ambazo zinafanya jitihada kubwa katika kutupatia huduma bora kabisa.” alisema
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya StarTimes nchini, Lanfang Liao amebainisha kuwa kuja kwa ligi ya Bundesliga ni muendelezo wa uboreshaji wa huduma zao ikiwemo maudhui waliyonayo katika ving’amuzi vyao.
“Leo ninayo furaha kubwa kuwaambia wateja wetu kuwa sasa ni rasmi ligi ya Ujerumani itawajia moja kwa moja kupitia dikoda zenu za StarTimes. Haya ni mafanikio makubwa ambayo tunajivunia katika kuendelea kuhakikisha kuwa watanzania wanaendelea kufurahia huduma za matangazo ya luninga kwa njia ya dijitali kwa gharama nafuu.” alisema Liao
“Tumeamua kuwaletea habari hii njema wateja wetu kuwa kuanzia tarehe 14 ya mwezi huu watakuwa na fursa wa kuangalia zaidi ya mechi 300 za ligi ya Ujerumani moja kwa moja. Mechi hizo zitaonyeshwa kupitia chaneli za ST Sport 2, ST Sports Premium na TBC2, hivyo kutoa uwanja mpana kwa watazamaji kuchagua mechi za kutazama. ” alisema
Aliendelea kwa kusema kuwa sababu kuu kwa kampuni yake kupata hakimiliki za kuonyesha ligi hii ni kutokana na huduma bora na nafuu wanazozitoa. Kwani wamiliki wa ligi hiyo wanaamini kuwa mamilioni ya waafrika ambao wengi wana vipato vya chini wanaweza kumudu gharama za ving’amuzi vya StarTimes.
“Kampuni yetu inaongozwa na faslafa ya kuhakikisha kuwa kila nyumba ya mtanzania inakuwa na uwezo wa kupata matangazo ya luninga kwa njia ya dijitali kwa gharama nafuu. Na hilo ni dhahiri kupitia gharama za ving’amuzi na vifurushi vyake ambavyo ni vya chini kuliko kampuni yoyote nchini.
Ni jambo ambalo tunajivunia sana na kwa kuwajali wateja wetu tumetoa ofa kuanzia tarehe 10 mpaka 14 Agosti kwa mteja atayelipia kifurushi chochote basi atapata tena kifurushi hichohicho kwa malipo yaleyale aliyolipia.
Kwa mfano kama utalipia kifurushi cha shilingi 12,000 basi utalipiwa tena kifurushi hichohicho bure kabisa, naomba watanzania wachangamkie ofa hii ya muda mfupi kabla ya kuanza kwa Bundesliga.”
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.