Baada ya kushindwa kupatikana kwa muafaka baina ya CHADEMA na Katibu wake Dr.Slaa na kupelekea chama hicho kumpatia likizo.
BARAZA Kuu la Chadema limeridhia Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa apumzike wakati chama hicho kikiendelea na mchakato wa Uchaguzi Mkuu baada ya kiongozi huyo kutofautiana nao katika uamuzi wa kumkaribisha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Baraza hilo jana lilipiga kura ya wazi huku likishauri kuwa endapo atafikiria kubadili uamuzi wake, atarejea kuendeleza safari ya chama hicho kuelekea Ikulu chini ya mwavuli wa Ukawa.
Uamuzi huo ulifikiwa jana wakati wa kikao cha Baraza Kuu kilichofanyika Jijini Dar es salaam, baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kueleza tofauti iliyojitokeza mwishoni mwa mchakato wa kumpokea Lowassa baina ya Dk Slaa na Kamati Kuu kiasi cha kumfanya Katibu Mkuu huyo kutohudhuria baadhi ya shughuli muhimu za chama.
Mbowe alisema Kamati Kuu ilifanya vikao kadhaa kutafakari ujio wa Lowassa na mashauriano ya muda mrefu ambayo hayakuwa rahisi kufikia uamuzi wa pamoja.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.