ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 14, 2015

AIRTEL FURSA YAANDAA SEMINA YA DARAJA LA MAFANIKIO KWA VIJANA MJINI MTWARA.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Salum Ally akifungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana.
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akizungumza wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana.

Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew Masatu akitoa mada kuhusu fursa mbalimbali zinazoweza kuwakwamua vijana kiuchumi, wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana.
Mkufunzi kutoka Mpango wa Anzisha na Boresha Biashara yako (SIYB) ulio chini Shirika la Kazi Duniani (ILO), Fidelis Madaha akitoa mada wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana.
Mkufunzi kutoka Mpango wa Anzisha na Boresha Biashara yako (SIYB) ulio chini Shirika la Kazi Duniani (ILO), Fidelis Madaha akitoa mada wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana.
Airtel Fursa yaandaa semina ya Daraja la mafanikio kwa Vijana Mjini Mtwara.

Vijana mkoani Mtwara wametakiwa kutumia fursa za uwepo wa nishati ya mafuta na gesi katika kukuza biashara zao na uchumi wa mkoa huo.
Wakizungumza mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya ujasiriamali mkoani humo, baadhi ya vijana hao wamesema kuwa fursa zilzizopo mkoani humo ni lazima ziwanufaishe vijana ili waendane na ukuaji wa uchumi wa mkoa huo.

Kampuni ya Airtel Tanzania, kupitia mradi wake wa “Airtel Fursa Tunakuwezesha” imewapatia mafunzo na kuwawezesha mitaji baadhi ya vijana wa manispaa ya mtwara kwa lengo la kuwawezesha kumudu uendeshaji  biashara zao na kukuza mitaji yao.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Salum Ally (kulia), akijadiliana jambo na vijana walionufaika na fursa za Airtel (kutoka kushoto), Iddy Salum Chilumba, Godfrey Frank Manjavila na Prisca George Chilumba baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kulia) na Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew Masatu.
Idd Abdallah ni mjasiriamali aliyenufaika na mafunzo hayo ambaye anasema kuwa kwa sasa amepata muongozo mzuri utakaokuza biashara zake na kuzifanya kwa weledi mkubwa zaidi.
“Hii ni fursa ya kipekee kwangu kama kijana na ninaishukuru sana Airtel kwa mafunzo yenye manufaa kwangu na vijana wenzangu wa hapa mtwara” Alisema Abdallah.

Nae mkuu wa wilaya ya Mtwara bi.Fatuma Ally, alisema “mafunzo haya yatapanua wigo wa ufahamu kwa vijana hawa ambapo aliwataka kujituma kwani fursa zipo nyingi mkoani humo.
“Mtwara kuna maeneo mengi sana yenye fursa kwa vijana kujiendeleza hivyo nawataka vijana kutumia fursa na mafunzo haya kuhakikisha wanajiendeleza kiuchumi” alisema mkuu huyo wa wilaya.

Hawa Bayumi ni Meneja Maendeleo ya Jamii wa Airtel, alisema hiyo ni fursa inatolewa na Airtel kwa lengo la kusaidia vijana kupata fursa ya kujiajiri na kupata mitaji kupitia mpango huo.
“Kwetu sisi Airtel tunaona ni fahari kuwawezesha wajasiriamali kwa mafunzo na mitaji ili waweze kuendeleza biashara zao na kukuza mitaji pia. Alisema Bayumi.

Ugunduzi wa gesi na mafuta mkoani hapa, vijana wanapaswa kujituma kwa kuongeza elimu na mitaji ili waweze kuwa sehemu ya wanufaika na kuondoka na hali ya kuwa watazamani wa tunu hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.