VURUGU zimezuka mchana wa leo zilizodumu hadi majira ya alasili wakati kiza kikiingia wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea na mkutano wake.
Baadhi ya Wanachama kwa idadi kubwa wameonekana waziwazi wakiandamana kuishinikiza Kamati Kuu ya Halmashauri ya CCM kulirudisha jina la mgombea wao Mhe. Lowassa.
ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA KILICHOJILI.
Barabara kuu iendayo jengo kuu la Chama cha Mapinduzi mkoani (CCM) Dodoma, (Nyerere road) imegeuka kuwa ukumbi wa mkutano kwa umati wa watu kufurika. |
Alasiri hii halmashauri kuu ya chama hicho ilifaanya kikao chake kupata majina matatu, halafu baadae leo jioni mkutano mkuu wa chama hicho unatarajiwa kukaa kupigia kura jina moja kati ya hayo matatu.
Yule atakayeibuka mshindi kati ya watatu hao ndiye atakaye kuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Ulinzi umeimarishwa. |
Kutoka juu, taswira ya eneo la viwanja vya ukumbi wa mkutano sanjari na maeneo jirani. |
Polisi wakiendelea kuwanasa wanaosadikika kufanya maandamano ambayo yanaashiria vurugu. |
Wanachama wa chama hicho wametapakaa kila kona. |
Majina matano yaliyopitishwa na Kamati Kuu ni Bernard Membe (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. John Magufuli (Waziri wa Ujenzi) Dk. Asha-Rose Migiro (Waziri wa Katiba na Sheria) January Makamba (Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia) na Balozi Amina Salum Ali (Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Tume ya Umoja wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa, Marekani)
Kufikia Jumapili, tarehe 12. Julai, Watanzania watakuwa wamejua ni nani atakayekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM kwa uchaguzi mkuu ujao.
PICHA NA MWANDISHI WA Gsengo blog ZEPHANIA MANDIA: DODOMA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.