MSEMAJI NO. 1
Kunazidi kucha huko kwa wahafidhina....magazeti ya leo yanafunua kile ambacho tumekuwa tunasema....Slaa bado peke yake anakataa ujio wa Lowassa chadema.....ametishia kurudisha kadi ya chadema iwapo mpango wa chama kumpokea Lowassa na kumpa ugombea urais utaendelea.......
Ngona tuone hii itaishia wapi?...
MSEMAJI NO. 2
Amini amini nawaambieni, kuna ukweli mkubwa tu kwenye hili na wala halikuanza leo. lilianza muda mrefu tu sasa linafukuta. Hamna awezaye kulipinga hapa kwa wale wandani ya chama. Slaa km kweli ni mpambanaji likitokea na arudishe kadi maana hamna jinsi nyingine, mtu timamu huwezi
kula matapishi.
MSEMAJI NO. 3
Hivi wa TZ tukoje?
Kwa nini tusingoje kupewa ukweli na wahusika, tunabaki na hisia tu, tukiamini habai za magazeti?
CCM ni chama kimoja, lakini tumeona changamoto zinazowakumba, itakuwa vyama vinne? Magazeti mengi yamekuwa yanajiandikia tu; mara hili linaandika hiki, lile linakanusha; mnawezaje kuamini maandishi haya?
Kwa nini tusisubiri, maana liwalo liwe, ukweli utajitokeza tu! Hivyo hakuna sababu ya ku-speculate!
MSEMAJI NO. 4
Hakuna kitu hatari kama ku corrupt media na kuwa na watu kama Ludo katika jamii wanaotutesa sasa hivi muda si mrefu watasikia kutoka kwetu.
Kichwa cha wendawazimu, kila kinyozi anataka aonyeshe staili yake. Wale wanajifunza na wale ambao ni hawajui kabisa!!!
MSEMAJI NO. 5
Kama sababu ya mtu au kikundi cha watu kuhama chama kimoja cha siasa kwenda chama kingine ni kutafuta kupata cheo peke yake, na siyo kushinikiza mabadiliko yenye tija kwa watanzania wote, uchaguzi utakuwa hauna manufaa makubwa kwa nchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.