MTIA nia kwa nafasi ya ubunge jimbo jipya la Kibamba kupitia tiketi ya ccm,Bw.Stanslaus Justine Maganga(26) ametangaza kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe Dr. Fenella Ephrahim Mukangara nae pia ni moja kati ya makada wa chama cha mapinduzi(ccm) wanaothubutu kutia nia kuwania kiti cha ubunge katika jimbo la Kibamba kupitia chama hiko.
Hali ya kisiasa jimboni humo imepamba moto baada ya watia nia hao wawili kuimarisha ngome zao kwa kupanga safu makini huku kila mmoja akijiwekea mikakati ya kumbwaga mwenzie katika kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika hivi punde.
Kwa habari za utafiti toka kibamba zinasema kuwa Bw. Maganga ambae ni mkazi halisi wa eneo hilo kuwa anakubalika zaidi hasa kwa vijana na wamama kutokana na kazi alizozozifanya kama kada wa chama na uwajibikaji wake katika shughuli za kuleta maendeleo jimboni humo.
Aidha aliongea kuwa alipata msukumo wa kutia nia baada kuona mapungufu katika utendaji,ubunifu,uadilifu na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo jimboni humo,ikiwemo miradi ya afya,maji na miundo mbinu.
Bw.Maganga amesema kuwa endapo atapita katika kura za maoni na anaamini atashinda ubunge hivyo atapeperusha vema bendera ya ccm na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kwa nia kuu ya kuleta maendeleo kwa wananchi.
Kada huyu ambae ana shahada ya kwanza katika biashara na uhasibu aliyoipata katika chuo kikuu cha KIU,katika maswala ya uongozi aliwahi kuwa Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo ,muasisi na Raisi wa taasasi ya kupambana na rushwa vyuo vikuu (Interuniversity anticorruption Associasion).
Pia amewahi kuwa mjumbe wa serikali ya mtaa wa Hondogo kata ya kibamba,mjumbe wa baraza la katiba akiwakilisha vijanakataya kibamba,mjumbe wa mkutano mkuu(ccm) kata ya kibamba.
Wakazi wa jimbo la kibamba wakimsikiliza mtia nia Bw.Stanslaus Justine Maganga wakati wa kutangaza nia. |
Kwa sasa Maganga ni mjumbe wa halmashauri kuu ya tawi la ccm maendeleo mtaa wa Hondogo kibamba na mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM kata ya kibamba.
Mwisho alimalizia kwa kusema endapo akichaguliwa na kushika nafasi ya ubunge ataenda kukomesha tatizo sugu la dhuluma za mashamba na ardhi ya raia maskini dhidi wajanja wachache wanaonufaika isivyo halali.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.