ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 12, 2015

SHINDANO LA ON LINE ART &SCIENCE LAPATA WASHINDI

Baadhi ya  washindi wakiwa wanakabidhiwa zawadi zao.
Baadhi ya  washindi wakiwa wanakabidhiwa zawadi zao.
Burudani ya sanaa ikiendelea.
Mmoja ya washiriki akiwa anaendelea kuchora wakati wa Sherehe hizo.
Picha ya Pamoja 

SHIRIKA la FASDO (Faru Arts and Sports Develepment Organization) leo hii limetoa zawadi kwa washindi wa shindano la Na Mimi Nipo- Online Arts and Science Competition katika ukumbi wa  kituo cha utamaduni cha Urusi nchini (Russian Tanzania Cultural Center).

Shindano hilo linalohusisha vipaji vya uchoraji, sanaa za mikono na ubunifu wa kisayansi lililozinduliwa mwezi Februari mwaka huu kwa lengo la kutambua vipaji vya vijana wenye umri kati ya miaka 12 hadi 24 limefikia kilele chake leo hii kwa kuwapata washindi sita, wawiliwawili kutoka katika fani za Uchoraji, Sanaa za Mikono na Ubunifu wa Kisayansi. 

Zoezi la kutoa zawadi kwa washindi hao lilihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Dr. Diodorus Buberwa, Mkurugenzi wa Kituo cha utamaduni cha Urusi nchini hapa, Alexander Tsykunov na wageni waalikwa.

Akizungumza na washiriki pamoja na wageni waalikwa katika Sherehe hizo Balozi wa Tanzania Nchini Ubelgiji aliwapongeza sana vijana kwa kuwa na vipaji vya hali ya juu na kusisitiza kuwa eneo hili la sanaa ya Uchoraji linatakiwa kupewa kipaumbele, aliongeza kuwa Tanzania sasa inatakiwa kuwa na maeneo zaidi kwa ajili ya kukuza sanaa hizi, na katika kuendeleza na kusapoti sanaa , Mh.Balozi Buberwa amechangia Tsh 1,000,000.

Washiriki walikuwa 27 lakini waliopata zawadi walikuwa ni washiriki 6 ambao walizingatia umri kati ya miaka 12 hadi 24 na washindi hao ni pamoja na Thomas Mwakilima, Anhony Tendwa, Primus Mapunda, Philipo Frolian, Cornelio Malya na Anderson Msangi washindi wote wamepata zawadi Dola 300.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.