ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 7, 2015

TENESCO KUSAIDIA KUINUA ELIMU KATIKA SHULE ZA VIJIJINI--MPENI DADA IREN MARK (2)

Meneja wa Tanesco kanda ya Dar es salaam na Pwani (katikati)
Wafanuyakazi wa Tanesco.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mafizi wakiwa wameketi chini.

*Tanesco yapania kusaidia sekta ya elimu vijijini

*Yatoa msaada wa madawati  100  shule ya msingi mafizi
 
NA VICTOR MASANGU, PWANI
 
SEKTA ya elimu hapa nchini kwa sasa  bado inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kuwepo kwa uhaba wa walimu,upungufu wa vitendea kazi,uhaba wa nyumba za walimu,ukosefu wa maabara pamoja na uhaba wa madawati hali ambayo inawalazimu baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari katika maeneo mbali mbali kujisomea wakiwa chini na miti pamoja na wengine wakiwa chini ya sakafu.
 
Hali hiyo inayoikabili sekta ya elimu inachangia kwa kiasi kikubwa kuzolota kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kutokana na mazingira ambayo wanasomea sio rafiki kwao hata kidogo hivyo wanajikuta wanafanya vibaya katika masomo yao tofauti na matarajio yao kutokana na kukabiliwa na changamoto hizo.
 
Katika baadhi ya shule za msingi pamoja na sekondari katika Mkoa wa Pwani bado hali hiyo imeonekana kuwa ni tatizo sugu kwa mudamrefu hususn katika maeneo ya shule za vijijini ambayo yamekuwa yakisahaulika katika kupata huduma mbali mbali zinazostahili katika kuboresha elimu.
 
 
Suala la elimu katika nchi ya Tanzania bado linaonekana kukabiliwa na changamoto nyingi ambazo  kwa namna moja hama nyingine baadhi yake serikali imeweza kujitahidi kwa hali na mali kuzipunguza lengo ikiwa ni kuhakikisha kwamba wanaboresha mambo ya msingi amabyo yataweza kuleta mabadiliko chanya katika elimu ya msingi pamoja na sekondari.
 
Kuwepo kwa changamoto hizo wakati mwingine kunachangia hata baadhi ya walimu kukata tamaa ya kujituma kwa bidii kuwafundisha wanafunzi kwani kwa upande  wao nao pia wanakabiliwa na kutokuwa na mazingira rafiki hususan nyumba za kuishi pamoja na kutopata mahitaji mengine ya msingi  ya kujikimu.
 
 
Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo Shirika la umeme Tanesco limeamua kujikita zaidi katika kuungana na juhudi za serikali katika  kuhakikisha wanaboresha sekta ya elimu ili kuwepa kuwa fursa wanafunzi  waweze kujisomea kwa bidii  katika mazingira ambayo ni rafiki kwa upande wao.
 
Uongozi huo wa shirika la umeme Tanesco kanda ya Dar es Salaam na Pwani imeamua kulivalia njuga suala la wanafunzi wa shule ya msingi iliyopo katika kijiji cha Mafizi Wilayani Kisarawe,Mkoa wa Pwani kwa kuamua kutoa sapoti ya msaada wa madawati 100 ili kuweza kuwasaidia wanafunzi ambao walikuwa wanakaa chini ya sakafu kwa kipindi kirefu bila ya kupatiwa msaada wowote.
 
Madawati hayo 100 yametolewa kutokana na viongozi wa Tanesco kuweza kubaini kuwepo kwa wanafunzi hao kusoma wakiwa chini ya sakafu, hivyo wakaona ni vema kutoa msaada huo ambao utaweza kuwa ni moja ya mkombozi mkubwa katika kuwafanya wanafunzi hao  waweze kujisoma katika  hali iliyo nzuri lengo ikiwa ni kuongeza kiwango cha ufaulu.
 
 
Hali hiyo ya wanafunzi wa shule ya msingi mafizi ya kukaa chini zaidi ya 100 imebainika mwaka jana wakati wa sherehe za mahafali ya darasa la saba ambapo waliweza kutoa changamoto hizo kwa mgeni rasmi Meneja mwandamizi  wa Tanesco Kanda ya Dar es Salaam na Pwani  Mahende Mugaya ambapo aliwaahidi kuwapatia msaada huo wa madawati.
 
Kilio hicho cha wanafunzi ambacho kilikuwa kinawasibu kwa  kipindi cha muda mrefu hivi karibuni kiliweza kubadilisha  hali ya uzuni na kuwa ya furaha kupita kiasi kutona na ahadi ambayo ilitolewa mwaka jana kutimzwa na shirika hilo la Tanesco na kuwapatia msaada huo wa madawati yapatayo 100.
 
Katika sherehe hizo za kukabidhi  madawati iliuzuliwa na wadau mbali mbali wa sekta ya elimu, viongozi wa serikali wa  Wilaya ya  Kisarawe, madiwani, wananchi pamoja na viongozi mbali mbali wa Tanesco kutoka Dar es Salaam na Pwani.
 
 Meneja mwandamizi  wa Tanesco  Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mahende  Mugaya anasema kwamba ana imani msaada huo wa madawati 100 katika wanafunzi wa shule ya msingi mafizi kutaweza kuleta mabadiliko makubwa katika kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi hao.
 
Mugaya anasema kwamba anatambua sekta ya elimu katika maeneo mbali mbali hususa na maeneo ya vijijini kuna changamoto nyingi hivyo kwa upande wao watajitahidi kwa hali na mali ili kuona ni jinsi gani kwa kushirikina na serikali pamoja na wadau wa maendeleo ya elimu  kujikita zaidi kuzisaidia shule mbali mbali hususani zile za vijijini.
 
Anasema kwamba vijana ndio Taifa la kesho hivyo wanafunzi wanatakiwa kupewa mambo muhimu ya msingi ili waweze kusoma kwa bidii na kuweza kuleta ukombozi ndani ya Taifa lao katika siku zijazo kutokana na elimu ambazyo wameipata, hivyo kama Tanesco tutazidi kutoa msaada katika elimu pale panapohitajika.
 
“Nakumbuka mwaka jana nilipatiwa mwaliko wa kuwa mgeni rasmi katika shule hii ya msingi iliyopo Mafizi, lakini katika risala yao kuikuwepo na  changamoto nyingi  hususan uhaba wa maji safi na salama, pamoja na  upungufu huo wa uhaba wa madawati hivyo nikato ahadi yangu na kiukweli nimeweza kuitekeleza ili kuweza kuunga juhuzi za serikali katika kuinua kiwango cha elimu,”
 
Pia mbali na kutoa msaada huo wa madawati 100 pia kutokana na wanafunzi hao pamoja na walimu kukabiliwa na kero kubwa ya kutokuwa na maji nimeweza pia kutoa msaada wa tanki kubwa la maji ambalo nina imani litaweza pia kuwasaidia kwa namna moja hama nyingine katika kuhifadhi maji ambayo yataweza kuwasaidia pindi pale wanapoyahitaji,”anasema Mugaya.
 
Kadhalika Mugaya anasisitiza kuwa Shirika la Tanesco linatambua mchangango mkubwa wa wateja wao hivyo ni vema wakashirikiana bega kwa bega kwa kile kidogo amabcho watakipata kuungana na jamii katika kuweza kuboresha miundombinu ya majengo ya walimu na madarasa ya wanafunzi ili kuweza kutimiza azma ya serikali katika kuboresha sekta ya elimu katika maeneo mbali mbali.
 
Pia Mugaya anasema kwamba kwa upande wa serikali pekee haiwezi kufanya kila kitu hivyo hakuna budi wazazi na walezi kwa kushirikina na wananchi kwa ujumla kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza kuisaidia kwa hali na  mali michangngo mbali mbali ambayo inakuwa inahitajika  katika kuendeleza maendeleo ya elimu.
 
Anaongeza kuwa kuna baadhi ya wananchi wengine wamekuwa hawataki kujikitza zaidi katika suala la kuchangia maendeleo ya elimu, hivyo wanapaswa kubadilika na kuwa na mtazamo chanya wa kuleta mabadiliko  ambayo yataweza kuisaidia kwa kiwango kikikubwa kwa wanafunzi wa sasa na vizazi vinavyokuja.
 
Katika hatua nyingine Meneja huyo anatoa wito na ushauri kwa walimu na wanafunzi kuhakikisha kuwa wanayatunza madawati hao, na waachane na tabia ya kufanya uharibifu wa miundombinu hiyo ambayo kwa upande wao imekuwa ni mkombozi mkubwa katika kulisongesha gurudumu la  sekta ya elimu.
 
Aidha anasema walimu nao wanatakiwa kuona umuhimu wa kufundisha pindi pale wanapomaliza katika vyuo mbali  mbali  na kupangiwa katika maeneo ya kufundishia vijijini wasikate tama na badala yake wajitolee kwa hali na mali kwani wanafunzi hao wanaomaliza vijijini ndio wanaweza kuwa ni viongozi hodari katika siku za mbeleni.
 
 
Madawati hao 100 yaliyotolewa katika shule ya msingi mafizi iliyopo Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani na Shirika la umeme Tanesco yamegharimu kiasi cha shilingi milioni nane na nusu.
 
Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo ya  msingi Mafizi Manyama Philipo akizungumzia kuhusina na hali hiyo anakiri kuwepo kwa changamoto hiyo ya madawati ambayo iliwalazimu wanafunzi zaidi ya  100 kujisomea chini ya sakafu hali ambayo imewapa wakati mgumu katika  kusoma kabla ya kupatiwa msaada huo.
 
Manyama anasema kuwa msaada huo waliopatiwa na Shirika la umeme Tanesco utaweza kuwasaidia wanafunzi wake kusoma sasa katika hali ambayo ni rafiki kwa upande wao tofauti na ilivyokuwa hapo mwanzao ambapo walikuwa wanasoka katika mazingira ambayo sio rafiki kwa upande wao.
 
“Awali ya yote napenda kuwashukuru Tanesco kwani wameweza kuona mbali na kuweza kutusaidia katika kulitatua hili jambo la madawati kwani mwanzi kwa keli ilikuwa ni aibu lakini Meneja Mugaya katika risala ya shule ameweza kuifanyia kazi kwa hivyo mimi nashukuru sana yeye pamoja na viongozi wote kwa kuunga juhudi za serikali katika kutatua chngamoto hizi,”anasema Manyama.
 
Aidha Manyama akifafanua zaidi anasema kwamba wanafunzi hao wakati wanajisomea chini ya sakafu pia walikuwa wanajikuta katika wakati mgumu kwani wanashindwa kuandika vizuri na wakati mwingine wanapatwa na ugonjwa wa mafua kutoka na sehemu ambaayo walikuwa wanakaa sakafu yake ilikuwa na vumbi sana.
 
Mkuu huyo mbali na kunaibisha changomoto za madawati pia anasema kwa sasa walimu wapo hatarini kupoteza maisha kutoka na vyoo walivyokuwa wanavitumia kutitia vyote kutokana na mvua ambazo zinaendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini.
 
Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo walimu hao kwa sasa wapo katika wakati mgumu kutokana na walimu wengine kwenda kujisaidia katika vichakani na wengine kwenda kujisaidia katika zahanati ya mafizi.
 
Manyama anafafanua kwamba vyoo ambavyo walikuwa wanatumia vyote vimetitia hivyo kuwafanya walimu hao kutumia mbinu nyingine ya kwenda kujisaidia porini na wengine kwenda kujisaidia katika zahanati ya mafizi.
 
“Kwa kweli ndugu mwandishi kwa sasa shule hii tunachangamoto ya vyoo kwani kutokana na mvua hizi ambazo zinaendelea kunnyesha kumesababisha vyoo ambazvyo walikuwa wanatumia walimu kiukweli naweza kusema vyote vimetitia kwani kimoja mabcho kilikuwa kimebaki nacho kimetitia hivyo tupo katika hali mbaya sana,” alisema Manyama.
 
Pia Mkuu huyo wa shule anaongeza kuwa  hata uko maporini wanapokwenda kujisaidia napo sio salama kwani wakati mwingine kunakuwepo na wanyama wakali ambo wanaweza kusababaisha madhara makubwa kwa walimu hasa katika nyakati za usiku usalama wao unakuwa ni mdogo.
 
Katika hatua nyinge Manyama anaiomba  serikali kujitahidi kwenda kuisaidiata  kwa hali na mali ujenzi wa vyoo vingine pamoja na wadau wengine mbali mbali wa maendeleo ili walimu hao waweze kuondokana na adha hiyo ya kutokuwa na vyoo ukizingatia na mvua bado inaendelea kunyesha.
 
Kwa upande wake mmoja wa walimu wanaofundisha katika shule hiyo Evelin Munisi  anasema  kwamba kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo hususan kwa walimu wa kike wanalazimika kwenda porini uku wakiwa na  majembe kwa ajili ya kujisaidia kitendo ambacho ni hatari kwa usalama wao.
 
“Kutokana na mvua hizi ambazo zinaendelea kunyesha zimesababish maafa makubwa sana kwa upande wetu kwani vyoo ambavyo tulikuwa tunavitumia vyote vimetitia, hivyo inatulazima sasa twende maporini kujisaidia uku tukiwa na majembe hali ni mabaya sana kwa kweli tunaomba tupatiwe msaada maana kwa hali hii tutapata wakati mgumu sana hasa katika kipindi hiki cha mvua,”anaongeza Manyama
 
Aidha katika hatua nyingine Mwalimu huyo akusita kugusia  kero ambazo wanakumbana nazo wanafunzi wa shule hiyo, sambamba na kuiomba serikali kuliangalia kati haraka  suala  hilo la walimu  kwa jicho la tatu ili wawe na molali wa kufundisha katika shule za vijijini ambazo zimekuwa mara nyingi zinakabiliwa na changamoto nyingi.
 
SHULE hiyo ya msingi Mafizi ambayo ilianzishwa mnamo mwaka 1973 licha ya kupatiwa msaada huo wa madawati lakini pia bado inakabiliwa na changamoto ya  ukosefu wa vyoo vya walimu na wanafunzi,nyumba za walimu,ukosefu wa maji, hivyo kunahitajika nguvu za ziada kupitia kwa serikali, wadau wa elimu, wabunge, madiwani pamoja na  wananchi kwa ujumla  lengo ikiwa ni kuiunga serikali  kutimiza malengo yake katika sera ya elimu hapa nchini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.