VICTOR MASANGU:PWANI
IMEELEZWA kwamba ongezeko la vifo vinavyosabishwa na ajali za pikipiki zinatokana na baadhi ya madereva kuwa na uzembe kutokana na kutozingatia sheria za barabarani ikiwemo kupakia abiria zaidi ya watatu almaarufu mishikaki kitendo ambacho ni hatari kwa usalama wa maisha ya watu.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Tanzania Mohameda Mpinga wakati wa kufunga mafunzo maalumu ya siku mbili ya maderava wa pikipiki katika Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani yenye lengo la kuwafundisha sheri mbali mbali za barabarani.
Kamanda Mpinga amebaisha kuwa kwa kipindi cha mwaka 2014 kulikuwa na ajali za pikipiki zipatazo 1449 katika nchi nzima ambapo kwa mwaka 2015 kuani=zia januari mpaka machi ajali ziliweza kupungua na kufikai idadi ya 668.
Kamanda Mpinga amebainsha kuwa kuhusina na vifo vilivyosababishwa na ajalili za pikipiki kwa kipindi cha mwaka jana 2014 amesema kuwa kumetokea vifo 218 ambapo kwa mwaka huu vifo hivyo vimeongezeka kwa kufikai vifo 220.
Aidha Mpinga amesema kwa sasa wanajitahidi kwa hali na mali kwa kushirikisna na wadau mbali mbali ili kuweza kuhakikisha wanatoa mafunzo kwa madereva wa pikpiki lengo ikiwa ni kuwaelekeza sheria na taraibu zote za barabarani.
“Kwa sasa katika kupambana na wimbi ili la ajali za barabarani hasa kwa ndugu zetu hawa wa boda boda tumejipanga kikamilifu katika kutoa mafunzo katika maeneo mbali mbali ya Tanzania ambayo ana imani yataweza kusaidia kwa kiwango kikubwa katika kupunguza wimbi la ajali,” alisema Mpinga.
Kadhalika Kamanda mpinga amewataka madereva hao ambao wamepatiwa mafunzo hayo kuyatumia vizuri pindi wanapofanya kazi zao na kuachan kabisa na tabia ya kupakia watu watatu kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha ya watu.
Baaadhi ya madreva wa pikipiki wakiwa wanatoka kwenye mafunzo. |
Kwa upande wake mwakilishi kutoka shirika la FIA Faundation kutoka nchini uingereza Monalisa Adhikali amewataka maderava hao wa pikipiki kuyatumia vema mafunzo waliyoyapata na kuwa wataendelea kushirikina kwa ukaribu kwa lengo la kuongeza elimu zaidi kwa maderava hao
Nao baadhi ya madereva wa wilyani Kibaha ambao wameshiriki katika mafunzo hayo wamesema kwamba mafunzo hayo yatakuwa ni mkombozi mkubwa kwa upande wao kwani kuna mamb mengine ya muhimu walikuwa hawayafahamu lakini kupitia mafunzo hayo yameweza kuwafungulia njia ya kuzitambua sheria na alma za barabarani
Mafunzo hayo ya maderava wa pikipiki katika Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani wamewashirikisha washiriki zaidi ya 100, ambapo yalikuwa na lengo la kuwafundisha sheria na alama mabali mbali za barabarani ili kuweza kupunguza wimbi la ajali.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.