Tangu internet iingie Tanzania, tumekuwa tukitumia mawasiliano yetu ya mtandao kwa uhuru sana na hilo kwa kiasi kikubwa limefanya maisha yetu ya mtandaoni yawe ya furaha, kwa jinsi watu wanavyoweza kupinga, kudanganya na kukosolewa, kufundishana, kuelekezana na hata kutaniana.
Lakini hata hivyo, kuna mengi mabaya ambayo yametokea na yanatokea kwenye mitandao ambayo sio ya kupendeza. Mfano ni kile kilichomkuta Betty Ndejembi (may she rest in peace) ambapo ulihuzunika sana na kifo chake. (Kama ujamjua huyu Binti soma bonyeza hii linkhttp://www.mwananchi.co.tz/Makala/Tunajifunza-nini-kifo-cha-Betty-Ndejembi-/-/1597592/2446702/-/jim9b9z/-/index.html)
Ukiachana na hilo, tusisahau suala la watu wanaoiba pesa kwa njia za simu kama ilivyomkuta Fid Q, au udanganyajifu wa kutumia majina ya watu maarufu kufanya utapeli kama ilivyowakuta Ridhiwan Kikwete, Zitto Kabwe na Lady Jay Dee ambapo watu walidai wanatoa mikopo kwa kutumia majina yao.
Tusisahau pia picha za ngono za wanavyuo na mitandao kama ZeUtamu ambayo imekuwa ikipost picha za kudhalilisha sana wahusika ukiachana na kwamba ni kinyume na maadili yetu.
Nadhani tumesahau haya yote haraka sana. Ni matukio kama haya ndio yaliyopelekea serikali ilete sheria mpya ya mtandao ili kuweza kudhibiti makosa yanayofanyika kwenye mtandao. Ni jambo jema. SANA. Sio jambo la kulipinga tu moja kwa moja ingawa kuna marekebisho tunayahitaji na muda zaidi kuweza kutoa maoni yetu.
Yote ya yote, kila mtu anahitaji uhuru na taarifa zake. Uhuru wa kutokuingiliwa na kuchukuliwa taarifa zake bila ridhaa. Uhuru wa kuchat na kutumia mtandao bila kuwa na wasiwasi kwamba anaweza kumuudhi mtu bila kukusudia akajikuta jela kabla ya saa6 mchana.
Katika makala hii, nitaelezea jinsi ambavyo unaweza kulinda taarifa zako zibaki kuwa zako peke yako kwa upande wa eseji, simu na mtandao.
Hii ni app nzuri sana na salama kama unataka message zako ziwe zako peke yako.
Faida zake ni pamoja na hizi:-
Faida zake ni pamoja na hizi:-
- Ina encrypt (au kufunga) message zako wakati ikiwa hewani kuelekea kwa unayemtumia, kiasi kwamba hakuna kinachoweza kuingilia katikati na kusoma message yako.
- Inalinda na kuifunga message yako kiasi kwamba hata kampuni ya simu unayotumia hawawezi kusoma message yako.
- Inaweza kutambua ni nani hasa aliyekutumia message.
- Message za nyuma zinabaki kuwa salama hata kama mtu akikuibia keys.
- Kusoma message zako mpaka password.
- Screenshot haiwezekani kupiga kwenye message ndani ya TextSecure.
Tukutane sehemu ya II siku ya Jumatatu
_____________________________________________________________________________
Support Team | RIGHT CLICK SOLUTIONS TANZANIA
P.O.Box 11503, Mwanza,Tanzania | Mob: +255 757 423421
Vijana Centre Building, Ground Floor | Room No.2 | Plot No. 11
Mlango mmoja street | Adjacent AAR Healthcare Hospital
E-mail: support@rightclicksolutions.co.tz | www.rightclicksolutions.co.tzFacebook: www.facebook.com/rightclicksolutionstanzania
“for more options”
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.