ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 5, 2015

MCHEZO WA STAND UNTD DHIDI YA MTIBWA SUGAR WAVUNJIKA DKK YA 37 STAND IKIONGOZA 1-0. KUMALIZIWA KESHO ASUBUHI

Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Shinyanga Benesta Lugola akizungumza kuhusu kuahirishwa kwa mchezo wa leo kati ya Stand United na Mtibwa Sugar kufuatia mvua kubwa kunyesha mjini Shinyanga na kusababisha uwanja kujaa maji.

Mchezo wa Stand UNTD dhidi ya Mtibwa Sugar toka mjini Morogoro uliokuwa ukichezwa kwenye dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga umeahirishwa hadi kesho saa mbili asubuhi kumalizia dakika 53 zilizosalia mara baada ya mchezo huo leo kuchezwa kwa dakika 37 kabla ya mvua kubwa iliyoambatana na radi kunyesha na kusababisha uwanja kujaa maji na hata vipimo vya uwanja kushindwa kuonekana. (BOFYA PLAY KUSIKIA KILICHOTOKEA)
Waamuzi wa mchezo wa Stand United V/S Mtibwa wakiwa na manahodha wa timu zote mbili.
Kikosi cha Stand United.
Mtibwa.
Krosi kuelekea lango la Mtibwa.
Mashabiki wa Stand United wakishangilia mara baada ya bao la kuongoza lililofungwa na Haruna Chanongo, hata hivyo mchezo huo utamaliziwa kesho asubuhi kwenye dimba la CCM Kambarage baada ya leo kuvunjika ikiwa ni dakika ya 37 kipindi cha kwanza, kufuatia mvua kubwa kunyesha mjini Shinyanga.
Hali tete mvua ikinyesha ndani ya uwanja wa Kambarage, mistari ya kutengenisha sehemu mbalimbali za uwanja imefutwa na maji ya mvua kubwa inayonyesha, mwamuzi hawezi kubaini makosa kutokana na macho kuwa na kazi ya ziada kwa uono hafifu, mpira hauendi mbali, pasi hazifiki wachezaji wakitumia nguvu nyingi.
Kandanda la kisasa halionekani mchezo umeharibika kutokana na mvua kubwa kunyesha.
Mpira umeshindwa kudunda mara baada ya kurushwa juu....Mwamuzi wa michezo akiwa na wasaidizi wake pamoja na manahodha wa timu zote akifanya majaribio kama mchezo uendelee au laa...
Ukaguzi ukiendelea kwenye milango ya pande zote.
Hali tete.
Mpita hauwezi kuchezwa.
Si salama.
Mchezo umeahirishwa dimbani hapa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.