Everton wameigalagaza timu ya Manchester united kwa kuwafunga goli 3-0 pale Goodson Park katika mchezo wa pili mfululizo kupoteza kwa kocha mdachi Louis van Gaal.
Man united walikosa nafasi nzuri ya kusawazisha goli la kwanza kwa nafasi murua kabisa ya Marouane Fellaini ambae alikua ni mchezaji wa wa Everton, japokua Man united walimilki sehemu kubwa ya mchezo kwa pasi fupifupi lakini walishindwa kabisa kutumia umiliki huo kutengeneza mabao kwa mechi ya pili mfululizo.
Wakati man united wakijiuliza kulikoni na wakidhani goli hilo moja litadumu hadi mapumziko everton walifanya shambulio moja kali la kushtukiza na kupata goli la pili na hadi mapumzo wakiwa wanaongoza 2-0.
Wenyenji walijikuta wakiongoza kwa goli 2-0 hadi muda wa mapumziko kwa magoli ya James McCarthy ambae ndio mchezaji bora wa mchezo huo aliefunga dakika ya 5 na kufuatiwa na John Stones dakika ya 35 na msumari wa mwisho ukishindiliwa na mchezaji alietokea benchi Kevin Mirallas dakika ya 74.
Japokua Van Gaal alimuanzisha Falcao baadae kumuingiza mchezaji ghali zaidi ligi kuu ya uingereza Angel Di Maria na mchezaji aliekuwa majeruhi Robin Van Persie lakini haikutosha kufanya asipate kipigo hicho.
Matokeo hayo yanaipeleka Everton hadi nafasi ya 12 na Man United kubakia Nafasi ya 4.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.