Airtel yazinduzia Ofa ya Internet BURE Tanzania
· Wateja kupata kifurushi cha bure cha hadi 50 MB kila siku asubuhi kuanzia saa 12 hadi saa 2 asubuhi
· Ofa hii ni kwa wateja wote wapya na wazamani kwa kupitia mtandao wa Airtel
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua kampeni kabambe inayotoa ofa ya internet ya BURE ijulikanayo kama “Na Like asubuhi” yenye lengo la kuwaunganisha watanzania wote kwenye huduma ya
internet na kuwawezesha kutumia na kufurahia huduma mbalimbali zinazopatikana kupitia Internet
Ofa hii inawawezesha wateja wa Airtel kupata internet ya bure ya hadi 50MB kuanzia saaa 12 hadi saa 2 asubuhi kila siku kupitia vifaa au simu zao zenye uwezo wa kutumia huduma ya internet
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Bw, Levi Nyakundi alisema” huduma ya internet ni muhimu sana katika kuendesha na kukuza shughuli za kijamii na kiuchumi.
Kadri unavyowaunganisha watu wengi kwenye huduma hii ya internet ndivyo tunavyowezesha uchumi wetu kukua kwa kasi. Kutokana na ripoti ya Mickinsey 2012 inayoelezea Power of Internet inasema Intaneti
inachangia takribani asilimia 21% kukua kwa pato la dunia katika maendeleo ya kiuchumi
Airtel tunaamini kwamba maendeleo ya kukua kwa pato katika nchi zilizoendelea yanawezekana kufikia kwa haraka kupitia ongezeko la watuamiaji wa huduma ya internet.
Kwa kuliona hili, leo tunayofuraha kuzindua ofa kabambe ya “Na Like asubuhi” itakayomuwezesha kila mtanzania kuunganishwa na huduma ya internet bila gharama yoyote aliongeza Nyakundi
Kwa upande wake Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya alisema “Hii itasaidia wateja wa Airtel na pia itaboresha nafasi yetu ya matumizi ya intaneti duniani ambayo kwa sasa ni asilimia 17% ukilinganisha na nchi zilizoendelea’
Kwa kupitia ofa hii watu wengi zaidi wataweza kuunganishwa na mtandao na kutumia huduma za mtandao sawa na matakwa ya serikali, pia huduma za kijamii kwa njia ya mtandao zitakuwa, wakulima watapata unafuu wa
kupashana habari za biashara zao, makampuni mbalimbali wataweza kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao wa intaneti aliongeza Mallya
Akiongea kuhusu kampeni hiyo Meneja wa kitengo cha huduma za internet bw, Gaurav Dhingra alisema”masaa ya asubuhi yatakuwa yakufurahisha kupitia huduma za mtandao wa Airtel kwa sasa. Wateja wanaotumia Airtel
watapata internet ya bure ya hadi 50MB kuanzia saa 12 hadi saa 2 asubuhi kila siku na kuweza kuitumia kuunganishwa na ndugu, jamaa na marafiki, kupata burdani, kupata taarifa za mambo yanayotokea duniani,
kuitumia kwa shughuli za kazi na nyingnine nyingi bila kuwa na gharama zozote
Ofa hii ni rahisi, na mteja wa Airtel ataipata awapo mahali popote nchini, ukiwa na line ya Airtel iliyosajiliwa na ikiwa una kifaa kinachokuwezesha kutumia huduma ya internet utaweza kuunganishwa moja kwa moja na kufurahia huduma hii ya bure ya internet kuanzia saa 12 asubuhi. Hakuna haja ya kupiga namba yoyote wala vigezo na masharti ya ziada tunachotaka kila mtanzania kufanya ni kufurahia Internet ya BURE kutoka Airtel Aliongeza Dhingra
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.