Picha ya Pamoja. |
Na
Mwandishi Wetu. Arusha.
MILESTONE
PARK Bar jijini Ausha wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager
NyamaChoma 2015 yaliyofanyiaka mwishoni mwa wiki katika Nanenane na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi milioni moja na Kikombe.
Nafasi ya pili ilichukuliwa Royal
Stop Over Baa ambayo ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 800,000/=,nafasi ya tatu ni Freedom
Baa ambayo ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/=,nafasi ya nne ni Capital 14 Baa aambayo ilizawadiwa Shilingi
400,000/= na nafasi ya tano ni QX Baa ambayo ilizawadiwa Shingi 200,000/-
Akizungumza na wakazi wa jiji
la Arusha waliofika katika mashindano hayo, Mnadhimu wa Jeshi la Polisi jijini Arusha,
Boniventure Mshongi, kwanza aliwashukuru kampuni ya Bia Tanzania(TBL)
kwa kubuni mashindano hayo ambayo ni mwaka wa nane sasa mfululizo yamekuwa yenye mvuto wa pekee ambayo yanawapa picha halisi wakazi wa Ausha kuwa wapi wanaweza kupata nyama choma
bora kutoka katika baa tano ambazo zimeingia fainali katika jiji la Ausha.
"Tunawapongeza kwa kutoa elimu kwa wapishi wa baa mbalimbali za jijini Arusha ambayo mliaanza nayo hapo awali tunaamini kwa kupitia hilo wapishi wetu wameelimika si kama mlivyowakuta na hilo tunawashukuru na tunawaomba muendelee nalo kwani mnaongeza ajira kwa jamii kama sikupunguza umasikini"
Pia Mshongi alizipongeza
baa tano zilizoingia fainali kwani wao ndio baa bora katika baa
zote zinazochoma nyama mkoani humo na aliwaomba waendelee kuilinda hadhi na sifa hiyo waliyopewa katika jiji
la Arusha na mwisho aliwapongeza mabingwa watetezi ambao wametetea vyema ubingwa wao, Bar
ya Milestone Park kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2015
na kuwaomba ambao hawakufanikiwa kupata nafasi hiyo wajiandae kwa mashndano yajayo ya
Safari Nyama Choma 2016.
Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa aliwapongeza mabingwa wa mwaka 2015, Miliestone Park Bar na pia aliwashukuru wote walioshiriki toka mchakato ulipoanza mpaka kufikia kumpata bingwa lakini pia aliwashukuru wakazi wa Arusha waliojitokeza kwa wingi kushuhudia nani anatwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma 2015 jijini Arusha.
Mwisho Edith
aliwaomba washiriki wote ambao waliopata zawadi wakatumie vyema zawadi walizopata kwa kuboresha majiko yao kwa mashindano yajayo ya
2016 lakini pia wakawe mabalozi wazuri wa bia ya Safari Lager kwenye biashara zao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.