VICTOR MASANGU, PWANI
WANAFUNZI na walimu katika shule ya msingi Mamlaka iliyopo katika halmashauri ya mji wa Kibaha Mkoa wa Pwani wanakabiliwa na changamoto uhaba na uchakavu wa miundombinu ya vyoo hali inayowapelekea kuwa katika hali ya hatari kutokana na hali halisi ya mazingira ya majengo wanayoyatumia kwa sasa.
Kuwepo kwa uchakavu huo wa miundombinu ya vyoo na uhaba wa matundu ya vyoo kunawafanya wanafunzi wengine kuishi kwa hali ya woga kwani vyoo vinavyotumika vipo katika hali mbaya ambayo inahatarisha kwa kiasi kikubwa usalama wa maisha yao ya kila siku.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Joyce Kilango amekiri kuwepo kwa hali hiyo ambapo amedai kwa sasa matundu ya vyoo vilivyopo ni matundu kumi tu, na mahitaji yanatakiwa matundu mengine 45 ili kuweza kukidhi mahitaji ya wanafunzi n walimu hao.
BOFYA PLAY KUMSIKILIZA MWALIMU MKUU
Kwa upande wao wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo akiwemo Jakson Ashili ,Felister Maendeka nao waliweza kutoa kilio chao kuhusiana na kero zinazowakabili ikiwemo suala la vyoo pamoja na uhaba wa maji safi hali ambayo wamedai pia wanaweza kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na kukithiri kwa uchafu.
WASIKILIZE WANAFUNZI
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha Silvester Koka ambaye alikwenda shuleni hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa mabati, mifuko ya simenti pamoja na viti katika ofisi ya walimu alikuwa na haya ya kusema katika kuboresha sekta ya elimu.
MSIKILIZE MBUNGE
Shule ya msingi Mamlaka iliyyopo halmashauri ya mji ambayo kwa sasa ina wanafunzi 772 kwa sasa bado inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uhaba wa madawati, upungufu wa madarasa sambamba na tatizo la maji ambalo limeonekana kuwa kero kwa wanafunzi pindi wanapokwenda kujisaidia.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.