ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 28, 2015

WALIMU WANAKWENDA KUJISAIDIA VICHAKANI KUTOKANA NA KUTOKUWA NA VYOO VYAO KUTITIA VYOTE

VICTOR MASANGU, KISARAWE PWANI
WALIMU wa shule ya msingi Mafizi iliyopo Wilayani Kisarawe, Mkoa wa Pwani wapo hatarini kupoteza maisha kutoka na vyoo walivyokuwa wanavitumia kutitia vyote kutokana na mvua ambazo zinaendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini.
Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo walimu hao kwa sasa wapo katika wakati mgumu kutokana na walimu  wengine kwenda kujisaidia katika vichakani na wengine kwenda kujisaidia katika zahanati ya mafizi.
Akizungumza na GSENGO BLOG shuleni hapo kuhusina na changamoto hiyo Mwalimu mkuu hiyo Manyama Philipo amesema kwamba miundombinu ya vyoo hivyo vipo katika hali mbaya sana ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa kwa  walimu hao.

Kwa upande wake mmoja wa walimu wanaofundisha katika shule hiyo Evelin Munisi  amesema kwamba kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo hususan kwa walimu wa kike wanalazimika kwenda porini uku wakiwa na majembe kwa ajili ya kujisaidia kitendo ambacho ni hatari kwa usalama wao kutokana na kuwepo kwa wanyama wakali katika maeneo hayo.
Aidha katika hatua nyingine Mwalimu huyo akusita kugusia  kero ambazo wanakumbana nazo wanafunzi wa shule hiyo, sambamba na kuiomba serikali kuliangalia suala la walimu  kwa jicho la tatu ili wawe na molali wa kufundisha katika shule za vijijini ambazo zimekuwa mara nyingi zikikimbiwa.
SHULE ya msingi Mafizi licha ya kukabiliwa na changamoto hiyo ya vyoo vyote kutitia pia wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama, pamoja na upungufu wa vyoo vya wanafunzi hivyo kuwalazimu wanafunzi hao  kwenda kujisaidia kwa  kupanga foleni na ambao wapo karibu na shule  kwenda kujisaidia nyumbani  kwao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.