|
Buluba Mabelele (kushoto) ambaye ni mdhamini wa Ligi ya Wilaya ya Busega maarufu kwa jina la Buluba Super Cup, akikabidhi mipira kwa Chama cha soka wilaya BUFA. |
NA ALBERT G. SENGO: BUSEGA MKOANI SIMIYU
CHAMA cha mpira wa miguu wilaya ya Busega (BUFA) mkoani Simiyu, kimepiga marufuku wachezaji wa vilabu vya Ligi kuu Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kutoshiriki Ligi ya Wilaya hiyo msimu huu iliyo maarufu kama BULUBA SUPER CUP.
Msimu uliopita baadhi ya vilabu vya ligi hiyo ya wilaya ya Busega, viliwatumia wachezaji wa timu ya Ligi kuu kutoka Stand United ya mjini Shinyanga na wachezaji wengine kutoka Ligi daraja la kwanza kwa vilabu vya Toto Africans na Mwadui Fc ambazo sasa zimepanda Ligi Kuu. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
|
Buluba Mabelele ambaye ni mdhamini wa Ligi ya Wilaya ya Busega maarufu kwa jina la Buluba Super Cup, akizungumza na wawakilishi toka vilabu 30 walio hudhuria mkutano wa Chama cha soka wilaya ya Busega BUFA kujadili mchakati kuelekea msimu mpya wa Ligi mwaka 2015-2016, likiwemo suala la uwezeshwaji toka kwa mdhamini. |
|
Sehemu ya wadau wawakilishi wa baadhi ya vilabu wilayani Simiyu mkoani Simiyu wakisikiliza kwa umakini kusanyikoni. |
|
Maswali na majibu ndani ya mkutano. |
|
Licha ya kuondoka na kombe bingwa wa Buluba Super Cup kwa mwaka 2015 atazawadiwa ng'ombe mnyama mwenye thamani ya shilingi laki 6, mipira miwili pamoja na seti ya jezi kwa timu. |
|
Vilabu vingi jimboni Busega vimekuwa na changamoto ya kuwa na viwanja vya kufanyia mazoezi ile hali vilabu vingi vikitegemea kudandia viwanja vya shule mbalimbali jimboni humo. |
|
Vifaa vya michezo navyo ni changamoto kubwa hivyo ujio wa wadhamini kama wa mdau wa soka Mr. Buluba umekuwa msaada kuwapunguzia makali ya mahitaji kwa timu mbalimbali jimboni haoa. |
|
Ukumbi wa mkutano kata ya Nyashimo ambayo ni makao makuu ya wilaya ya Busega mkoani Simiyu. Jumla ya timu 16 toka katika kata mbalimbali zitashiriki Ligi ya wilaya (BUSEGA SUPER LIGUE) msimu wa 2015-2015. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.