UVCCM YAMCHARUKIA WAZIRI NYALANDU
Dar es salaam Machi 25 2015, Umoja wa vijana wa CCM (UVCCM), umemjia juu waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu kwa madai ya kwamba amekua akitoa kauli za kejeli kupitia mitandao ya kijamii na kuungwa mkono na baadhi ya marafiki zake.
Kauli hiyo ya UVCCM imekuja siku chache baada ya Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM), Abdulraham Kinana kumtaka Waziri Nyalandu aende kutatua migigoro ya wananchi wanaoishi jirani na hifadhi.
Alisema badala ya Waziri huyo kufanyia kazi ushauri wa Kinana, yeye ameibuka kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kuanza kutoa kauli za kejeli.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Bw. Sixtus Raphael Mapunda alisema badala ya Waziri Nyalandu kwenda na kasi ya Kinana na sekretarieti ya CCM yeye amekua bize kujibizana kwenye mitandao.
“UVCCM inamtaka aende akatatute migogoro ya hifadhi na wananchi inayowatesa Watanzania kwa muda mrefu sasa, kila eneo la hifadhi kuna migogoro na wananchi”.
Umefika wakati sasa maliasili za Tanzania ziwanufaishe na kuwatumikia Watanzania badala ya hali ya sasa ambapo wananchi wanakuwa wanaumia kwa mali zao za asili nchini kwao wenyewe.
Haiwezekani tukalinda tembo na twiga wetu vizuri na tukashindwa kuwatetea Watanzania wanaonyanyasika katika maeneo ya hifadhi na tukatoka mbele za watu na kupaza sauti eti mmefanya kazi nzuri ya ulinzi wa tembo na mkaona hiyo ndio sifa” alisema Mapunda.
Pia aliongeza kuwa utendaji mzuri wa kazi ni kuwalina Tembo na Twiga na kutatua migogoro ya wananchi kwani vyote lazima viende pamoja na kumtaka Waziri Nyalandu kuiga mfano aliouonesha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi ambaye alikwenda haraka kusikiliza na kutafutia ufumbuzi kero za ardhi katika mikoa ya Dodoma, Manyara na Arusha baada ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Kinana kubaini uwepo wa tatizo kubwa la migogoro hiyo, ni jambo la kupongezwa na kuigwa na viongozi wengine wa serikali. "Kutafuta mchawi badala ya kutekeleza wajibu husika kwa kiongozi wa serikali ni kujiondoshea sifa za kuendelea kuwa mtumishi kwa wadhifa unaoutumikia," alisema.
UVCCM inampongeza Katibu Kinana kwa ziara yake inayoendelea kufanywa kwenye mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoahidiwa katika ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010-2015 na kuimarisha CCM.
"Kazi hii kubwa inayofanywa na Kinana na wajumbe wake imekirejeshea heshima kubwa Chama cha Mapinduzi katika kipindi hiki cha siasa za ushindani wa vyama vingi.
"Ili kufikia malengo ya kuwatumikia Watanzania kwa tija isiyo kifani, UVCCM chini ya ndugu Kinana na sekretarieti yake ni kutatua shida na kero za wananchi," alisema.
Aliongeza kuwa, UVCCM inaunga mkono kauli ya Kinana anayoitoa katika ziara yake inayoendelea hivi sasa mkoani Kilimanjaro ya kuhamasisha viongozi kutoka maofisini na kwenda vijijini kusikiliza kero za wananchi na kuzifanyia ufumbuzi, kwani kiongozi ni mfano wa kuigwa lazima aoneshe njia ili wanaomfuata wasijikwae.

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.