ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 26, 2015

MADHEHEBU YA KIKATORIKI YAASWA KUTOWAGAWA WATANZANIA KWA MISINGI YA KIDINI.

NA PETER FABIAN, NANSIO.
WANANCHI na waumini wa madhehebu ya Kikristo mkoani Mwanza wametakiwa kutafakari kwa umakini waraka wa maaskofu na wachungaji unaosambazwa katika makanisa na matamko ya viongozi hao ambayo yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani na kuanza kutugawa kwa misingi ya kidini.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa CCM mkoa wa Miraji Mtaturu wilayani Ukerewe klatika ziara yake ya kikazi alipokutana katika kikao cha viongozi na wajumbe wa halmashuri kuu ya chama hicho pia alipowahutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi hapa mjini Nansio.
Mtaturu alisema kuwa ni vyema Maaskofu na Wachungaji wakarejea kuisoma upya Katiba inayopendekezwa badala ya kutumia nafasi zao za kiroho kuwahamasisha waumini wao kufanya maamuzi wanayoyataka hata kama yanavishiria vya kuanza kubaguana kidini na kitabaka huku wakitambua ni kumkosea Mungu.


“ Maaskofu na Wachungaji ni watu wanaoheshimika na kuaminiwa hivyo wasitumie udhaifu wa baadhi ya waumini na wananchi ambao hawana tabia kusoma katiba inayopendekezwa na kuwapotosha ili waamini wanachokisema wao ndio kilicho sahihi.” Alitahadhalisha.

Katibu alisema kuwa wananchi waisome Katiba inayopendekezwa kuanzia ibara ya kwanza hadi ya mwisho hakuna kipengere kilichoandika Mahakama ya Kadhi lakini pia hata wajumbe wa Bunge maalumu la Katiba hawakujadiri juu ya uanzishwaji wa mahakama hiyo na badala yake walishauri jambo hili liwe mswada ambao utawasilishwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.

“ kinachofanywa kwa sasa kupitia matamko na waraka unaosambazwa makanisani na kusomwa kwa waumini kupitia Maaskofu na Wachungaji hauna ukweli wowote, labda waeleze kuwa wanaajenda yao ya siri na baadhi ya vyama vya siasa walivyokubaliana navyo.” Alisisitiza.

Aliongeza kwamba viongozi hao ni vyema wakaacha kuvaa majoho na kuhubiri siasa makanisani badala ya kushughulikia mambo ya kiroho kama ilivyowapendeza kuwa watumishi wa Mungu ikiwa wao ni kioo cha jamii kukosoa viongozi na waumini wanaokwenda kinyume na mambo ya kiroho.

Wito wangu kwa Watanzania wakiwemo viongozi wa madhehebu ya dini zote ni vyema tukashirikiana kuhakikisha tunailinda misingi yote ya amani na utulivu iliyopo huku tukiwanyooshea vidole na kukataa baadhi ya watu wanaotaka Taifa litumbukie katika nyongo ya vurugu na kusambaratika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.