ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 11, 2015

'FICHUA UKATILI WA KIJINSIA UFIKIE MALENGO YAKO' MKOA WA MARA WANENA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Mkuu wa mkoa wa Mara Kapteni Anseri Msangi akihutubia kwenye maadhimisho ya Siku ya mwanamke duniani ambapo katika mkoa wa mara yaliadhimishwa wilayani Tarime chini ya usaidizi wa Shirika la kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia la KIVULINI lenye makazi yake jijini Mwanza.
Akina mama wakiwa katika maandamano kuingia eneo la kusanyiko katika viwanja vya shule ya sekondari 
Akinamama katika maandamano kuingia eneo la kusanyiko na ujumbe 'Fichua ukatili wa kijinsia ufikie malengo yako ya maisha'
Akinamama toka Halmashauri mbalimbali za wilaya mkoa wa Mara zimeshiriki maadhimisho hayo ambayo mkoa umeadhimisha wilayani Tarime.
Maandamano.
Akinamama nguvu moja.
Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI Yassin Ally akitoa takwimu.
Wilaya za mkoa wa Mara zinaongoza kwa vitendo vya ukatili wa Kijinsia nalo Shirika la Kupinga na Kuzuia ukatili wa Kijinsia KIVULINI linatumia mbinu mbalimbali za kiubunifu ili kukabiliana na hali hiyo kwa kubadili mifumo.

Takwimu za Mwaka 2010 zilizotolewa na Demographic Earth Survey zinaonyesha kuwa mkoa wa Mara unaongoza nchini kwa tatizo la ukatili ambapo ni asilima 66.4 vitendo vya ukatilikwa nchinzima vinatendeka katika mkoa huo. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
Sehemu ya kusanyiko.
Akina mama mkoa wa Mara na wilaya zake.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mara Kapteni Anseri Msangi na jopo lake la meza kuu wakipata maelezo ya miradi mbalimbali ya akinamama na akinababa wa vikundi mbalimbali ambao wamekuwa bega kwa bega kutoa elimu ya kupinga ukatili mkoani Mara.
Maelezo toka kikundi cha ujasiliamali na uzalishaji bidhaa kwa akinamama. 
Kikundi cha Nyumba Salama hutumika kuwahifadhi mabinti walio kimbia vitendo vya ukatili na kukeketwa majumbani kwao, wanawake hao hufundishwa mbinu mbalimbali za ujasiliamali na kujiendeleza kiuchumi.
Bidhaa za kikundi cha ujasiliamali cha 'Nyumba Salama' kutoka mkoani Mara.
Pamoja na kupewa maelezo toka vikundi mbalimbali vilevile mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Mara Kapteni Anseri Msangi alitumia muda wake kuuliza maswali ya changamoto pamoja na kutoa ushauri kwa vikundi vya ujasiliamali. 
Huduma ya elimu kaya kwa kaya, makundi na vipeperushi mbalimbali vya kufikisha ujumbe mitaani pamoja na mbinu mbalimbali hutolewa na KIVULINI.
Kusanyiko likisikiliza ujumbe.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.