Mmoja wa Maafisa wa Kampuni ya Sola ya Mobisol aktoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari |
Tushusheni vifaa na tumfungie mteja wetu wa Kwanza Joseph Kiyenze , ni maafisa wa Kampuni ya Mobisol Ltd tawi la Kanda ya Ziwa lililopo jijini Mwanza |
Ofisi za Kanda ya Ziwa zilizopo eneo la Kanyama Kata ya Kisesa Wilayani Magu mkoani Mwanza. |
Vifaa vya kazi ya kufungia umeme wa Sola |
Ndani ya Ofisi ya Kanda ya Ziwa |
Tunatoa elimu ya kuwashawishi wateja wetu vijijini na maeneo yasiyo na umeme. |
NA PETER FABIAN, MWANZA.
WANANCHI wa maeneo ya Kata ya Igoma waliokaa zaidi ya miaka 25 bila kuunganishiwa huduma ya Nishati ya umeme wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) wamefurahishwa na ujio na upatikanaji wa umeme wa Sola unaounganishwa kwa wananchi na Kampuni ya Mobisol Ltd ya jijini Arusha.
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa mtambo wa umeme kwa mwananchi wa eneo la mtaa wa Kishiri ‘B’, Joseph Kiyenze, Mtendaji wa Kata ya Igoma, Philbert Magana, alisema kuwa maeneo mengi ya Kata hiyo hayana umeme wa Tanesco hivyo ujio wa Kampuni ya Mobisol Ltd, inayosabaza na kuunganisha umeme wa Sola (Nishati ya jua) kwa wananchi wanaonunua umepokelewa kama mkombozi katani.
Magana alisema kuwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 25 wananchi wa maeneo ya Igoma na Kishiri yenye mitaa 26 yamekuwa katika giza kutokana na wananchi kuomba kuunganishwa na Tanesco kwa miaka zaidi ya 10 kupata umeme wa Grid ya Taifa lakini imekuwa hakuna majibu na jitihada za kufikishia na kuwaunganishia umeme jambo ambalo limekuwa ni kero ya muda mrefu isiyokuwa na ufumbuzi.
“Wananchi wenye mahitaji na uwezo wa kuunganisha umeme wa Sola wa mitambo ya Kampuni ya Mobisol iliyopiga hodi na kuwasilisha ombi lao katika kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Igoma (WDC) na kukubaliwa na wenyeviti wa mitaa 26 za Kata, watapata fursa ya maendeleo kwa kutumia umeme wa Sola na kusaidia kutoa huduma kupitia vifaa vya Kiteknolojia kwa kupata habari na mawasiliano,”alisisitiza.
Awali katika hafla ya kumkabidhi mteja wao Kiyenze, Meneja Masoko wa Kampuni ya Mobisol Ltd, tawi la Mwanza, Albert Msengezi, alisema ujio wa kampuni yake na Nishati ya umeme wa Sola kwenye maeneo mbalimbali ya vijijini na mijini yasiyokuwa na umeme wa Tanesco ni kutokana na kufanyika kwa utafiti na kubaini kuwepo changamoto na mahitaji halisi kwa wananchi wasiofikiwa na huduma ya nishati ya umeme wa Tanesco.
“Mitambo ya Sola inayotumia jua na kuzalisha umeme wa Wati 30, 80, 120 na 200 kwa garama ambazo wananchi wanaweza kumudu na kuunganisha mitambo ya sola kulingana na mahitaji ambapo wateja wataomba kuunganishiwa kwa mkopo na kwa malipo ya awali, wiki na mwezi baada ya maobi ya mteja kukubaliwa na kufungwa mkataba jinsi ya kulipa,”alisema.
Msengezi alisema kwamba vifaa vya mitambo ya Sola wanavyofunga kuzalisha umeme vimekidhi ubora wa kimataifa kwa kuidhinishwa na Shirika la Viwango la Taifa (TBS) ambapo vinadumu kwa miaka zaidi ya 25 na garama zake kuwa nafuu zaidi ambapo Kampuni itaunganisha mitambo yake kwa bei ya mkopo na kuuza kwa wateja wake na Kampuni hutoa motisha ya Sh. 15,000/- kwa watu wanaopeleka wateja wapya .
“Mitambo yetu iko katika viwango tofauti ambapo wati 30 zinawasha taa 5, wati 80 zinaweza kuwasha taa 10 na TV moja , wati 120 zinaweza kuwasha taa 15, Komputa moja na TV na wati 200 zinaweza kuwasha taa 20, Jokofu moja na TV na kwa mteja atakayeguswa na kupata huduma ya mitambo yetu afike katika ofisi za Kampuni za Mobisol zilizopo eneo la Kanyama Kata ya Kisesa wilayani Magu,”alisema.
Kwa upande wake mwananchi Kiyenze aliyeunganishwa na mtambo wa kuzalisha umeme wa sola wa wati 80 hupewa betri moja (55AH) taa tatu ndogo za ndani , tochi moja na chaji ya simu na TV ndogo ambapo alisema kwamba kutamwezesha kuangalia habari kupitia runinga, redio na kumwezesha kuchaji simu na kuwa na mawasiliano na kuwa balozi wa kuwashirikisha majirani zake juu ya mitambo na vifaa vya Kampuni ya Mobisol.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.