ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 6, 2015

WAHANDISI WA SEIKALI ZA MITAA KIJITAFAKALI ILI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA

 
NA PETER FABIAN, MWANZA.
WAHANDISI walioko katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa, wametakiwa kujitafakari kwa kina ili kutekeleza majukumu yao yatakayosaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa jamii kutokana na miradi mingi kutumia gharama kubwa katika utekelezaji wake.
Akifungua mkutano mkuu wa mwaka waWahandisi wa Serikali za Mitaa jana jijini Mwanza, Mgeni rasmi katika mkutano huo, KatibuTawalawaMkoawaMwanza, Faizal Issa, hotuba yake iliyosomwa na mwakirishi wake, NdaloKulwijira, alisema kwamba wahandisi wazingatie taaluma yao katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa jamii.
“Taaluma ina umuhimu mkubwa kwa taifa na jamii, hivyo ni vyema mkatekeleza majukumu yenu kwa weledi mkubwa wakati wa kutekeleza maradi ya maendeleo inayotumia gharama kubwa ilikuwezesha kutoa huduma kwa jamii kwa muda mrefu na kwa ubora unaotakiwa,”alisema.
KwilwijiraalisemakuwaAssociatin of Local Government Enginners in Tanzania (ALGETA) ni Jumuiya ambayo kazi zake niza kitaalamu zaidi hivyo ni vyema mkajadiliana kwa kina  na kubadilishana uzoe na kuwa ma mfumo bora na  kutimiza wajibu wenu na dhamana mliyonayo katika taifa na halmashauri zenu ilikukabilia na changamoto za utekelezaji miradi mbalimbali ya jamii.
Kwilijira nimeeleza kwamba Wahandisi wanaoshiriki mkutano huu wote wanatoka Serikali za mitaa (TAMISEMI),ambao nimamizi wanaosimami utekelezaji wa miradi ya miundombinu inayotekelezwa na wananchi katika ngazi ya mamlaka za serikali za mitaa vikiwa ni vyombo vilivyo karibu na wananchi
“Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali imekuwa ikionyesha mojawapo ya sababu za Halmashauri kupata Hati zisizoridhisha na chafu kutokana na miradi kutosimamiwa kikamilifu ikiwa ni i ile miradi ya maji, miundombinu ya majengo na barabara hali hii imeanza kudhibitiwa kila mwaka,”alisema.
Serikali inawataka watumishi wote ikiwemo wahandisi kuweka mikakati inayotekelezeka  na isiyokinzana na sheria na maadili ya utumishi ambapo serikali imejipanga kuwasaidia kadiri inavyowezekana ili kufanikisha azima yake ya Serikali  ya awamu ya nne ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.
“Nawaasa Wahandisi wote kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretalieti za Mikoa na Hata Wizara kuwatumikia wananchi kwa uadilifu wa hali ya juu kwa taratibu za maadili ya utumishi wa umma pamoja na kuwa na jukumu la kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kujiletea maendeleo kwa ustawi wao binafs kwenye maeneo yao,”alisisitiza.
Awali Rais wa ALGETA Taifa, Mhandisi Ezekiel Kunyaranyara, kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano huo, alisema mkutano huo wa kikatiba wa Jumuiya hiyo utajadili “Utoaji Huduma Bora za Kihandisi Kwa Maendeleo ya Jamii” katika Sekta ya maji, barabara na majengo ikiwemo mitambo ya umeme.
Mhandisi Kunyaranyara, alisema kuwa mkutano huo ni halali kutokana na Jumuiya hiyo ya ALGETA kusajiliwa mwaka 2007 na kupata usajili Na 14878 na kuwa na wanachama 453 ambao ni wahandisi na wafundi wasanifu 531 ikiwa lengo kuu ni kuwaleta pamoja wataalamu wote wanaofanya kazi chini ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Sekretalieti za Mikoa na Wizara ya TAMISEMI.
“Mkutano huu umelenga pia kusaidia wanafunzi wasichana katika shule za sekondari kusoma masomo ya Sayansi kwa kutoa msaada wa vitabu, pia kutoa msaada wa madawati 100 katika shule mojawapo ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza na wajumbe kupata fursa ya kutembelea mradi wa barabara za Mawe iliyokamilika,”alisema.
Mkutano huo wa siku mbili pia utajadiliana jinsi ya kuongeza ushiriki wa watoto wa kike kupenda kusoma masomo ya Sayansi yatakayo pelekea wao kuwa wahandisi baaada ya kuhitimu ili kuongeza wahandisi wakike na kutekeleza majukumu ya kulijenga taifa bora lenye kasi ya maendeleo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.