ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 14, 2015

KITU KIPYA KABISA KUTOKA KWA ISHA MASHAUZI “NIMPE NANI” …NI ZOUK RHUMBA LENYE UTAMU WA MASAUTI

ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Wala hakosei kusema ‘kujua kazi ni raha’. Isha Mashauzi anashuka tena kivingine na wimbo mpya kabisa uitwao “Nimpe Nani” unaodhihirisha kuwa anaijua vema kazi yake.

Hii ni ‘single’ yake ya pili nje ya taarabu ukiiacha wimbo wake wa  kwanza “Nimlaumu Nani” uliopigwa katika miondoko ya rhumba. 


“Nimpe Nani” ni wimbo unaoelea kwenye miondoko ya zouk rhumba lakini ukikolezwa kwa mbali na vionjo vya mduara.


Wimbo huo wa dakika tatu na nusu ambao umerekodiwa katika studio za C9 Records chiniya producer C9 Kanjenje, Kinanda kimepigwa na Kali Kitimoto na C9, magitaa ya bass na solo yamepigwa na Babu Bomba wa Malaika Band. 


Sauti zote tamu unazozisikia humo ni za Isha Mashauzi kasoro sehemu ndogo sana isiyozidi sekunde 5 iliyo itikiwa na Easy Man.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.