ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 27, 2015

HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA YATOA MAFUNZO KWA WEVYEVITI WA MITAA YOTE YA KATA 12 WALIOCHAGULIWA WILAYA YA NYAMAGANA

Kutoka juu eneo la ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
NA PETER FABIAN, MWANZA.
HALMASHAURI ya Jiji la Mwanza, imetoa semina ya mafunzo ya masuala ya msingi na ujuzi juu ya uendeshaji wa serikali za mitaa kwa wenyeviti wake wote wa mitaa waliochaguliwa hivi karibuni.

Akifungua semina hiyo ya siku moja jana iliyofanyika katika ukumbi wa Jiji , Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida, alisema kuwa baada ya wenyeviti kuchaguliwa hivi karibuni, Halmashauri imeona ni vyema ikawapa maelekezo ya utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa wananchi katika mitaa yao.

“Wenyeviti wote sasa mjikite kuwatumikia wananchi wote katika mitaa yenu bila kuwabagua kwa itikadi zenu za kisiasa na badala yake muelekeze kuwatumikia kwa misngi isiyokuwa ya kisiasa kwa kuzingatia uendeshaji wa shughuli za serikali za mitaa,”alisisitiza.

Hida alisema kuwa kutokana na baadhi ya wenyeviti kuwa wageni katika ngazi hii ya uongozi ni aliwahasa kutumia fursa hiyo ili kuwawezesha kutambua na kusimamia majukumu yenu kwa jamii mnayoiwakilisha ikiwa ni pamoja na kufanya kazi hii bila kuegemea katika msingi wa siasa jambo ambalo linaweza kupelekea kuwa na kubaguana katika uetekelezaji wa kazi hii.

“Kwenye mitaa yenu vipo vyanzo vya mapato vya Halmashauri hivyo ni vyema mkavibaini na kuhakikisha tunashirikiana katika ukusanyaji wa mapato ili kuwezesha Jiji kurejesha asilimia 20 ya mapato katika Kata na hatimaye kufika katika ngazi ya mitaa yenu,”alisisitiza.

Mkurugenzi Hida aliwaeleza washiriki kuwa kutokana na Kasi ya ukuaji wa Jiji kuna baadhi ya maeneo ya mitaa yao yataweza kuwa katika mipango ya uanzishwaji wa miji midogo ya kisasa na hivyo ni vyema wakawaandaa wananchi katika kuipokea na kukubaliana na mipango ya Jiji kwa kuzingatia sheria za mipango miji ili kurahisisha utekelezaji wake.

Naye Mkufunzi wa semina hiyo, Mtaalamu wa masuala ya Utawala bora, Donald Kasongi, kutoka shirika la Links, akitoa mafunzo hayo aliwaeleza serikali za mitaa ni vyombo vya utawala vilivyo karibu zaidi na wananchi ambavyo vinasimikwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuimarisha demokrasia katika utoaji  wa huduma  kwa jamii.

Kasongi alisema kuwa, kwa mujibu wa Katiba ibara 146, Serikali za Mitaa ni vyombo vya haki na vyenye mamlaka ya kushiriki na kushirikisha wananchi katika kupanga  na kutekeleza shughuli za maendeleo na utoaji wa huduma katika sehemu zao.

“Kazi kubwa ya mwenyekiti wa mtaa ni kuitisha mikutano mkuu wa wananchi wote, kusikiliza na kuchukua kero za mtaa wake kutoka kwa wananchi na kupeleka katika kikao cha Maendeleo cha Kata (WDC), kupanga na kukubaliana katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo uanzishaji wa miradi hiyo,”alisema Kasongi.

Wito wangu teendelee kujifunza na kushirikiana na watendaji wa mitaa, madiwani, watendaji wa Kata na Ofisi ya Mkurugenzi ili kuwezesha kufikisha taarifa zitakazosaidia wananchi kushiriki katika juhudi za maendeleo na kuwezesha pia Halmashauri kutekeleza yale ambayo yamekusudiwa ili kutoa huduma kwa wananchi na si kuegemea katika siasa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.