ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 18, 2014

WAZIRI KAMANI AFUNGUA SEMINA YA VIONGOZI WA WAVUVI WILAYANI UKEREWE

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Dkt Titus Mlengeya Kamani (Mb) akitoa hotuba ya ufunguzi wa Semina yaViongozi wa Wavuvi (BMU) iliyofanyika Hotel ya Monach Nansio Ukerewe, chiniya udhamini wa mfuko wa Pensheni wa PPF. 
"Ndugu Meneja wa Kanda, napenda kuupongeza Mfuko wa Pensheni wa PPF ambao unatekeleza mojawapo ya sera zake ya kuhakikisha sekta isiyo rasmi inafikiwa kama ilivyo kwa sekta nyingine za uchumi hapa nchini. Hii itaongeza pato la Taifa hivyo kuzidi kuboresha maendeleo ya Watanzania kwa ujumla na kupunguza umaskini. Napenda kuwaambia kuwa kwa kuandaa semina hii muhimu katika eneo ambalo mimi mwenyewe nalisimamia imenipa faraja sana kwa kuona jinsi Mfuko huu wa PPF unavyowajali sekta zote za uchumu wa nchi. Hongereni sana."
Kwa mujibu wa Meneja wa Kanda ya Ziwa Ndugu Meshack Bandawe (pichani aliyesimama) alisifia Mahudhurio ya semina hiyo akisema kuwa yanadhihirisha kuwa kuna mwamko wa jamii ya watanzania kuhusiana na masuala ya hifadhi ya jamii unaendelea kukua na kuimarika. 
Wanasemina wakichukuwa data muhimu.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Mary Onesmo Tesha akitoa neno la shukurani pamoja na kukazia umuhimu wa mafunzo yanayotolewa kwa wananchi na vikundi kuhusu mifuko ya pensheni.
Huku wakizidi kuongezewa maarifa na manufaa ya semina husika, tayari wavuvi zaidi ya 2000 wameshajiunga na PPF. 
Pia wanasemina hao walipata fursa ya kuuliza maswali pamoja na kufanya majadiliano ikiwa ni sehemu ya kupima uelewa. 
PPF imeweka mikakati ya kuwafikia zaidi ya wavuvi 4000 katika wilaya ya Ukerewe. Aidha, PPF mapema mwakani ipo katika mkakati wa kufanya utafiti kwa ajili ya kuangalia jinsi ya kukopesha vikundi mbali mbali vya ujasiriamali vilivyopo katika sekta zisizo rasmi.

IFUATAYO NI SEHEMU YA MWISHO YA HOTUBA YA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE. DKT TITUS KAMANI (MB):-
Ndugu Viongozi na Wawakilishi wa Wavuvi, nitoe rai kwenu kuipa nafasi semina hii muhimu ili muweze kuangalia wapi panahitaji kuboreshwa kwani hii itawasaidia kupiga hatua katika uvuvi wenu. Kwani kwa taarifa nilizonazo zoezi hili la kujiunga na PPF limefanikiwa sana ila changamoto kubwa ikiwa ni uwasilishaji wa michango yenu PPF.

Napenda kuwahamasisha kuwasilisha michango kwa wakati katika Mfuko wa PPF kwani ni Mfuko mkongwe ambao vile vile umezidi kuboresha mifumo ya Tehama kwani sasa kupitia simu ya mkononi unaweza kuwasilisha mchango wako kupitia M-pesa,Tigo Pesa na Airtel money. Kwenu nyie kutokana na asili ya kazi yenu ya uvuvi njia hizi ni muafaka zaidi katika kuwasilisha michango yenu kwa wakati.

Ndugu Viongozi na Wawakilishi wa Wavuvi, kwa kuwa nimeambiwa kuwa hapa tulipo kuna viongozi wa wavuvi wasiopungua 50, hii inaashiria jinsi mlivyolipa uzito suala hili la kujua manufaa yaliyomo ndani ya Mfuko wa PPF na hatimaye muweze kujiunga. Sasa napenda niseme hivi, nyinyi viongozi mliofika hapa mchukue jukumu la kusimamia zoezi hili katika maeneo yenu ya kazi ili wavuvi wengi waweze kukwamua maisha yao kutoka uvuvi duni kwenda uvuvi wa kisasa. Hivyo basi mnapaswa kuangalia kwa makini mambo yafuatayo:-
·                    Kila kiongozi awe na orodha ya wavuvi walioko katika kituo chake ambao tayari wamesajiliwa
·                    Kila kiongozi lazima afahamu kilammoja anachangia kiwango gani aidha kwa wiki au kwa mwezi na kuweka kumbu kumbu kwa ajili ya mrejesho
·                    Kila kiongozi awe na namba za simu za wavuvi walioko katika kituo chake
·                    Kila kiongozi ajiridhishe kila mvuvi aliyejisajili awe na kitambulisho cha uanachama cha PPF
·                    Kila kiongozi kuhakikisha anafahamu wavuvi wote wasiojisajili na PPF au Mfuko wowote
·                    Viongozi wote wachukue jukumu la kuhamasisha wavuvi wote walioko katika vituo vyao wajiunge na kuchangia katika Mifuko ya hifadhi ya jamii kama Mfuko wa Pensheni wa PPF
·                    Vile vile nitoe agizo kwa viongozi wote na wawakilishi wa wavuvi wafanye kazi kwa karibu na ofisi ya PPF kanda ya Ziwa  kwa ajili ya ufanisi na manufaa  ya wavuvi kwa ujumla

Ndugu Meneja wa Kanda, baada ya kusema hayo, sasa naomba niwakabidhi jukumu hili la kutoa semina kwa viongozi hawa wa wavuvi ili mkawasajili wavuvi waweze kufaidika PPF ili kuboresha maisha yenu na ustawi wa jamii.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.