ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, December 14, 2014

WAUMINI WA HINDU WAMLALAMIKIA RC MURONGO WATISHIA KUMUONA WAZIRI MKUU PINDA NA RAIS Dkt. JAKAYA KIKWETE MWANZA.

Askari wa zimamoto wakidhibiti moto uliowashwa mbele ya maduka ya wafanyabiashara kupitia vurugu zilizopata kutokea jijini Mwanza.
WAUMINI wa Madhehebu ya Hindu wamelalamikia kauli ya hivi karibuni, iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Murongo, akiagiza uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutowaondoa wafanyabiashara wadogo “Machinga” katika eneo la Makoroboi wanaofanya biashara jirani na nyumba za kuabudia (Ibada).

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa msikiti wa Sirigur Singh Sabha, Manjit Singh, alieleza kuwa, kauli hiyo ya RC Murongo imeleta utata na kusababisha eneo la barabara ya Tample iliyokuwa katika ujenzi kushindwa kukamilishwa sanjari na waumini wa misikiti iliyopo eneo hilo kushindwa kupita kirahisi na kupata usumbufu wakati wa kwenda kwenye Ibada.

Manjit alieleza kwa masikitiko kwa niaba ya waumini wa dhehebu lake pamoja na wale wa miskiti jirani ya Sanathan Hindu Temple, Baaps Swaminarayan inayomiliki pia Shule ya Chekechea ya Rajendra iliyopo ndani ya msikiti huo katika eneo maarufu la Mtaa wa Makoroboi ambalo kwa sasa limevamiwa tena na machinga baada ya kuondolewa na Halmashauri ya Jiji.

“Tunasikitishwa kweli na kitendo cha machinga hao kurudi eneo hili kwa madai ya idhini na kauli iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Murungo aliyehamishiwa mkoani hapa akitokea Mkoa wa Arusha hivi karibuni,”alisema.

Kiongozi huyo alifafanua kuwa chini ya uongozi wa RC Evarist Ndikilo tulikaa na viongozi wa serikali Wilaya ya Nyamagana, Halmashauri ya Jiji la Mwanza, viongozi wa makundi ya Machinga kupitia Shirika la Umoja wa Mashinga Mkoa wa Mwanza (SHIUMA) na kufikia makubaliano kuliacha wazi eneo hilo la misikiti tu ambalo sasa limevamiwa tena na machinga.

 “Manjit alisema katika zoezi la kuwaondoa zilipelekea baadhi ya vijana ambao badae ilibainika siyo machinga kuchoma baadhi ya sehemu za nyumba za ibada katika eneo hilo na kuharibu kwa kurusha mawe na hata kuharibu mali zingine za waumini ikiwemo kuchoma moto magari kabla ya vurugu hizo kutulizwa na kikosi cha askari Polisi wa kikosi cha FFU toka kambi ya Mabatini.

“Sisi ni wazaliwa na raia wa Tanzania wenye asili ya Ki- asia lakini kupitia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunao uhuru wa kuabudu katika madhehebu yetu, lakini pia hatupashwi kubaguriwa kwa rangi na makabila zaidi ya kushirikiana na kudumisha umoja, amani wa taifa letu kama ilivyo ilivyoshauri na waasisi wetu kuwa dhambi ya kubaguana tukiikubali tutamalizana wenyewe,”alisisitiza.

Aliongeza kwa kunukuu maneno ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere ambaye alikuwa muasisi wa Taifa hili "Tukianza kubaguana kwa rangi na makabila kitakachofuata ni dini zetu, dhambi ambayo aitaishia kuaacha salama na huo ndo utakuwa mwanzo wa kuulizana wewe umetoka Mkoa gani kisha tunatumbukia kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe hapo ndo mwanzo wa kutoweka amani na umoja wa Taifa letu"alieleza kwa masikitiko.

Mwenyekiti huyo alieleza kuwa kutokana na hali hiyo ilivyo sasa katika eneo hilo ambalo miundombinu ya barabara ilikuwa ikiboresha kwa ujenzi imesimama pamoja na ukarabari wa baadhi ya majengo ya misikiti yaliyokuwa yameharibika wakati wa vurugu za kuwaondoa machinga na kusimama pamoja hata kusababisha waumini kuhofia usalama wao wakati wa kwenda kwenye ibada.

Waumini wametoa wito kwa viongozi wa juu wa serikali kuliangalia kwa umakini na weredi suala hilo na kulishughulikia ili kuepuka kutokea umwagaji damu na vurugu katika eneo hilo, pia kumuomba RC Murongo kutengua kauli yake na kuwaondoa machinga hao ikiwa pia kuomba radhi waumini wa misikiti hiyo kwa usumbufu wanaoupata kabla ya kufikisha malalamiko yao kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Rais Dkt. Jakaya Kikwete .

Naye Mwenyekiti wa SHIUMA, Ernest Matondo alieleza kuwa machinga hawana ugomvi na uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na waumini wa madhehebu ya Hindu kutokana na makubaliano ya awali ambayo yalikuwa ya malidhiano na mafanikio yaliyopelekea machinga kupangwa katika maeneo kumi yaliyotengwa kwa utaratibu na kwa sheria za Mipango Miji.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Halifa Hida, akizungumza na MTANZANIA jana alisema kuwa sasa hana jibu la kupingana na kauli ya RC juu ya hali ya machinga hao kurejea Temple Makoroboi na kufanya shughuli zao kiholela kwa madai ya machinga hao kuruhusiwa na Murongo, badala yake atalifikisha suala hilo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kutokana na azimio la awali la kuwapanga kutolewa na kikao hicho.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.