MWANZA.
MAWAKILI wa kujitegemea zaidi 50 wanachama wa Chama cha Tanganyika Law Society (TLS) kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wametoa msaada wa ushauri wa kisheria na kusikiliza na kujibu maswali ya malalamiko ya wafungwa na watuhumiwa walio mahabusu wapatao 2,000 katika Gereza Kuu la Butimba la Mkoani Mwanza.
Akizungumza na waandhishi wa habari jana baada ya kuzungumza na wafungwa na mahabusu katika makundi tofauti, mwakirishi wa Mwenyekiti wa TLS, Wakili Costantine Mtalemwa, alieleza kuwa zoezi hili ni sehemu ya maadhimisho ya Sheria ambayo hufanyika kuanzia Desemba mosi hadi siku ya kilele ya Desemba 11 kila mwaka nchini kote.
Mtalemwa alisema kuwa mawakili hao wa kujitegemea TLS wametembelea gereza hilo na kukutana na wafungwa na watuhumiwa ambao wako mahabusu kwa makosa ya jinai, madai na kujibu maswali yao ya msingi na kutaka kujua haki zao nasi kutoa ushauri wa kisheria na kuchukua baadhi ya kero zao katika
mashauri yanayowakabili.
mashauri yanayowakabili.
“Lengo ni kuona jinsi ya kuwasaidia zaidi kisherialakini mengine ni kufikisha katika vikao vya utendaji vya pamoja kati ya watendaji wa Mahakama, Mawakili na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kanda, lakini pia lamsingi ni nikuona jinsi ya kuwa na uwakirishi kwa mujibu wa Katiba ya nchi”alisema.
Mtalemwa akizungumzia watuhumiwa wengi wa makosa ya jinai waliokutana nao alisema wameongelea zaidi jinsi ya mashauri yao kutoka katika vyombo vingine vya utendaji vinavyochelewa kusikilizwa na kutolewa maamuzi kutokana na kutokamilika kwa upeleleze wa kesi kwa wakati, walalamikaji kuhama na mashahidi kutoonekana na kukamilika wakati wa mashauri.
“Baada ya msaada huu tulioutoa leo tutawasilisha kwa iongozi wetu na kuchambua yale ambayo tumesikiliza, wale watakaoonekana kuwasimamia ili kusaidia mashauri yao kufutwa kutokana na kukaa muda mrefu bila kusikilizwa, wanaohitaji kutatiwa rufaa na watuhumiwa ambao ni wa kesi za madai kuyawasilisha katika kikao chetu cha pamoja cha utendaji mwaka huu,”alisema.
Aliongeza kuwa baada ya kuonana na wafungwa kumekutwa changamoto nyingine kwa wafungwa wanawake baadhi wanawatoto wadogo wa kuanzia mwaka mmoja hadi miwili, wengine wamefungwa kwa kuiba ghrasi tatu za thamani ya Sh. 11,000/= au nguo za thamani ndogo wanafungwa miezi sita hivyo tumeona wangeweza kupata adhabu mbadala.
Naye Wakili wa Gereza la Butimba Mkoa wa Mwanza, Sajini Meja Rehema Sawaka, alisema kuwa kilichofanyika ni msaada wa kisheria kutoka kwa mawakili upande wa utetezi kwa mahabusu na watuhumiwa wa makosa ya madai na jinai katika Gereza la Butimba ambapo zaidi ya walioonwa ni 2,000 wamepata fursa ya kuwaeleza sheria inavyosema na kuchukua hoja za malalamiko yao.
“Mawakili wamechukua yale ambayo wanadhani yanahitaji masaada wa kisheria ili kuwasaidia kupata haki wafungwa kuweza kukatiwa rufaa na watuhumiwa walio mahabusu kuona jinsi gani kesi zao jinai zinasikilizwa na zilizokosa kukamilika kwa kutokamilika kwa upelelezi basi zifutwe na za madai zitolewe adhabu mbadala ikiwa ni vifungo vya nje, kulipa faini au kufanya kazi za usafi na mazingira ofisi za serikali,”alisema.
Sawaka alisema makundi yaliyosikilizwa na mawakili wa utetezi ambao ni wakujitegemea wa Chama TLS ni wale wenye makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha, wizi, madai na mauaji ambapo ya mauaji yamechukua muda mrefu katika upelelezi ambapo wapo watu wanaokabiliwa kwa mauaji tangu mwaka 2004, 2006 hadi leo lakini kesi zao hazijasikilizwa kabisa lakini hiyo pia ni tatizo la rushwa linachangia dhamana kuwa kikwazo kwa mahabusu.
“Sheria inataka kesi isikilizwe haraka na kutolewa uamuzi, lakini humu ndani ya Gereza Kuu la Butimba idadi ya watuhumiwa walioko mahabusu imekuwa ikipungua kila wakati baada ya kesi zao kusikilizwa, lakini pia kwa sasa kesi zimekuwa zikisikilizwa na mahakimu na majaji kwa wakati, labuda chache ambazo ushahidi wake uchelewa na mashahidi kukosekan.
Wito wangu kwa ndugu na jamaa wa watu waliofungwa magereza na walio na tuhuma za makosa mbalimbali walio mahabusu wametakiwa kutowatenga na badala yake kuwatembelea na kukutana nao, lakini kwenda kukutana na mawakili wa TLS au kuonana na mratibu wake wa mambo ya kutoaa msaada wa kisheria bure, Linus Amri ili kuwasaidia ndugu na jamaa zao wenye makosa na vifungo gerezani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.