ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 22, 2014

TIMU YA WATAALAMU NA WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA KUTEMBELA JIJI LA MWANZA BAADA YA KUSAINI MKATABA MWISHONI MWA JUMA LILILOPITA

Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM) katikati, Mwenyekiti wa Mji wa Youngpu kutoka Jiji la Shaghai China, Ma Xiaohua (kulia) na Mkurugenziwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Halifa Hida (kushoto) wakisaini Mkataba wa Mahusiano kati ya Jiji la Mwanza na Mji rafiki wa Youngpu wa Jiji la Shaghai China jijini Mwanza.
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Stansalaus Mabula (CCM) wa pili kulia, Mwenyekiti wa Mji wa Youngpu wa Jiji la Shaghai China, Ma Xiaohua (kulia) wakionyesha Hati za Mkataba wa Mahusiano walizosaini mwishoni mwa juma lililopita Jijini Mwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji, Halifa Hida na nuyma yao ni ujumbe wengine kutoka China na Jiji la Mwanza.
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Stansalaus Mabula (CCM) wa pili kulia,
Mwenyekiti wa Mji wa Youngpu wa Jiji la Shaghai China, Ma Xiaohua (kulia) wakikabidhiana Hati za Mkataba wa Mahusiano walizosaini mwishoni mwa juma lililopita Jijini Mwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji, Halifa Hida na nuyma yao ni ujumbe wengine kutoka China na Jiji la Mwanza.
Picha zote na Peter Fabian wa GSENGO BLOG.

NA PETER FABIAN, MWANZA.

TIMU za wataalamu na kundi la wawekezaji kutoka Mji wa Youngpu Jiji la Shanghai China kuja kutembelea Jiji rafiki la Mwanza ikiwa ni kuendeleza na kudumisha uhusiano.

Hatua hiyo inatokana na ujumbe wa viongozi na watendaji sita kutoka mji rafiki wa Youngpu uliopo jijini Shanghai China kutembela Jiji la Mwanza na kusaini Mkataba wa malidhiano ya uhusiano mwishoni mwa juma lililopita na kushuhudiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Jiji la Mwanza.

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida,  alisema kuwa awali katikati mwezi Agosti mwaka huu ujumbe wa Jiji la Mwanza ulitembelea Mji huo katika Jiji la Shanghai na uliongozwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo (Pwani), Meya wa Jiji la Mwanza, Stansalus Mabula, Mkurugenzi Hida na Afisa Uhusiano wa Jiji, Joseph Mlinzi.

 “Mkataba huu utasainiwa na Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM), Mwenyekiti wa Mji rafiki wa Youngpu, Ma Xiaohua na Mimi Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza mbele yenu Madiwani wote, watumishi na ujumbe wa Mji rafiki, ambapo awali kabla ya kutiliana saini ujumbe huo ulitambulishwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ofisini kwake,”alisema.

Hida alisema kuwa makubaliano waliyoahidi kuyatekeleza ya kuja kusaini mkataba wa kufufua upya  uhusiano ambao yalionekana kufifia kati ya Mji huu wa Youngpu na Jiji la Mwanza yalianzishwa mwaka 2009  kabla ya leo kuwekeana saini mkataba wa makubaliano mapya Desemba 19 mwaka huu jijini hapa.

Mkurugenzi Hida, aliyataja makubaliano waliyotiliwa saini mkataba kuwa  yamelenga maeneo manne muhimu, kwanza ni eneo la Teknolojia na Mawasiliano kwa kuzingatia wao wako juu, pili ni kuja kuona fursa za uwekezaji na kubadilishana uzoefu na kuingia ubiya na wafanyabiashara wa Jiji hili na Mkoa wa Mwanza kupitia  Chama cha TCCIA.

Hida alitaja eneo la tatu ni eneo la Mipango Miji ambapo wataleta wataalamu kuja kufanya mazunguzo na wataalamu wa Jiji la Mwanza kutusaidia kulipanga na kuriboresha katika eneo la Central Business District (CBD) , uanzishwaji Miji mipya  ya kisasa katika maeneo ya Luchelele Kata ya Mkolani na Kata ya Igoma na nne ni eneo la utali kwa kutangaza vivutio , utamaduni na Hifadhi za taifa za Sanane na Serengeti.

Kwa upande wake Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM) aliwaeleza Madiwani, Watumishi wa Jiji hilo na ujumbe huo, kuwa mkataba huo wa mahusiano utatekelezwa kwa miaka mitano katika maeneo hayo, lakini urafiki utaendelea kama awali japokuwa kwa sasa umeboresha zaidi na utatoa fursa kwa pande mbili kutembeleana na kubadilishana uzoefu.

“Uhusiano huu pia umelenga kutusaidia na utawezesha Jiji kunufaika zaidi kutokana na rafiki zetu hawa kuwa katika kiwango kizuri kiuchumi duniani na kupiga hatua kubwa kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya mawasiliano na teknolojia, sekta ya viwanda na uwekezaji wa majengo ya kitega uchumi na ujenzi wa miundombinu ya barabara ikiwemo usafirishaji,”alisisitiza.

Naye Mwenyekiti wa Chines People’s Political Consultative Conference (CPPCC), Ma Xiaohua, kutoka Mji huo alisema kwamba katika ziara ya Uongozi wa serikali ya Mkoa na Jiji la Mwanza walipowatembelea waliipokea na kuahidi kuyatekeleza yale waliyokubaliana kwa vitendo baada ya kukaa, pamoja na kuleta makubaliano hayo kuja kuyasaini ili kuanza utekeleaji wake.

Ujumbe kutoka Jijila Shanghai China uliongozwa na Mwenyekiti Xiaohua, Katibu Mkuu wa CPPCC, Hu Yaoliang, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara katika Mji wa Youngpu,  Zheng Zuohua, Mkuu wa Idara ya Utamaduni, Mkuu wa Idara ya Mipango Miji na Upendezeshaji Miji, Xu Feng, Mkuu Msaidizi wa Idara ya Majeno na Usalama, Yang Benhe.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.