MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU KWA COLLEGE NA SCHOOL ZA UDSM YAPAMBA MOTO.
* SJMC (School of Journalism & Mass communication) wanaongoza kilele cha group A
* COSS (College of Social Science) wanaongoza kilele cha group B
* Mechi zingine nne kuendelea leo hadi Jumamosi
Mashindano ya mpira wa miguu kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yanayojulikana kama Airtel UNI255 yanayoshirikisha wanafunzi wote wa schools na Colleges zilizopo chuoni hapo yameendelea kwa kasi yakiwa leo yameingia siku ya tatu toka kuanza kwake huku baadhi ya washiriki wakijichukulia ushindi na kuongozo msimamo wa mchezo huo na wengine kuendelea kusuasua .
Akiongea kuhusiana na mwenendo wa mashindano hayo kwa sasa Waziri wa michezo wa jumuiya ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam STANLRY JULIUS alisema "Mashindano ya mwaka huu yamekuwa na mvuto wa kipekee hasa kutokana na wadhamini wetu Airtel kutupatia vifaa vya kutosha na kwa namna moja yameongeza hari sana kwa washiriki wote
Hadi sasa kinara wa kundi A ambao mechi zao zinachezwa pale katika viwanja vya ndani chuo kikuu cha Dar es salaa ni SJMC (School of Journalism and Mass Communication) alicheza mechi mbili na kushinda zote na kujitengenezea pointi 6 na huku akiongoza kwa kuwa na bao 5 za kufunga.
Kundi B ambao mechi zao zinazochezewa katika viwanja vya chuo kikuu za Mabibo maarufu kama Mabibo Hostel linaongozwa na COSS (College of Social Science) ambapo imecheza mechi 3 ikashinda moja na kutoa sare ya bila kungana mechi 2. Kwa matokeo hayo wanapointi 5 na goli 2.
Mashindano haya ya Airtel UNI255 yanaendelea tena leo na yatafikia tamati siku ya jumamosi kwa fainali itakayokutanisha mshindi wa kundi A na kundi B na baadae Airtel imeandaa tamasha maalum la vipaji maalum kwa wanafunzi wa chuo hicho litakalofuatiwa burudani kali toka kwa wasanii maarufu wa kizazi kipya nchini akiwemo shilole, Ney wa Mitego, Roma na wengineo. Aidha katika kilele cha tamasha hilo Airtel itazindua kwa wanafunzi wa chuo kikuu huduma ya UNI255 itakayowawezesha kuwasiliana , kuperuzi internet kwa gharama nafuu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.